Naomba ifanywe kwa dharura: Napendekeza kuanzia Jumamosi iwe ni marufuku mtu kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa/ barakoa/ scarf

Wazo zuri.

Maana wengine wakiongea wanarusha sana MATE
 
Who are you?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataalamu wananichanganya wengine haisaidii,wengine muhimu kuvaa wengine hapana.........
 
Barakoa inatakiwa ivaliwe kwa masaa yasiyozidi 4 tu,, so Elimu pia ingeenda sambamba na hilo
 
Kufunika uso ni suluhisho dogo Sana Kwa tanzania, unajua huwezi kufikia hapo kabla hujachukua hatua zingne jamani
Funga makanisa, funga masoko Yote, funga kariakooo na kusimamisha usafiri wa umma, hizo ndio hatua kuuuu, huuu ugojwa unaambukiza kwa asilimia 80 kupitia mikononi, na kugusana huko kwenye hiyo mikusanyiko niliyoitaji ningumu kuepusha kugusana na ni ngumu kuzuia mikono isishike kitu huko kwenye usafiri, Baar na kanisani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi simuuungi mkono, huwezi kuzuia hilo kwa Tanzania yenye idadi ya mamilioni hamsini kuwa kila mtu azuie uso wake popote aendako ni ngumu Sana kikubwa, Baar zifungwe, minada ifungwe, makanisa yafungwe, masoko yafungwe na usafiri wa umma ufungwe watu watumie hata baisker na pikipiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono wazo la kuvaa barakoa,hii ni kwa kila mtu na asievaa abakie ndani kwake,hii ni hatua muhimu sana,na ya pili ni kupima abaria wote wanaopanda mabasi kituo cha mabasi ya mikoani ili kuinusuru mikoa ambayo haina maambukizi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi za fremu utalipa wewe au unaongea tu
 
Ugumu wa kuvaa barakoa ni upi na urahisi wa kufungia watu biashara zao ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…