Nakuunga mkono.
Serikali imechelewa na inachelewa sana kutoa tamko la kujikinga zaidi ya kunawa mikono.
Watu wote tungeanza mapema kukinga midomo na pua ingesaidia kupunguza maambukizi kwa njia ya chafya na kukohoa.
Unakuta basi zima hakuna hata MTU mmoja aliyefunika USO. Watu wanaingia msikitini na kusujudi bila kuvaa maski wakati anapogusa ardhini ndipo mwngine alipogusa dk chache zilizopita.
Pia watu wanunue gloves wavae kwani zinafaa kuosha kwa sabuni na kuvaliwa tena na tena. Mana sio kwamba zinatumika hospitalini Bali ni kugusa vitu na kisha zinaoshwa na sabuni kisha MTU asiye na uwezo anavaa tena kuliko kuuza vitu sokono mikono mitupu na mdomo na pua wazi.
Watoa huduma wote wavae maski kwa kweli mana huenda bidhaa wanazouzia watu wanazipigia Chafya au kukoholea halafu wateja wananunua.
Wauza vyakula na vinywaji nao wavae maski na mikononi wavae gloves.
Sent using
Jamii Forums mobile app