huu ndio original
NAOMBA KIBALI CHAKO
Moyo wangu mtiifu tuli umetuwa kwako
Kwangu huna upungufu yote nimekupa heko
Kwa mapana na marefu wa kukupinga hayupo
Jambo moja nina hofu nataka ridhaa yako
Kwahiyo nakuwarifu nipate nasaha zako
Nakuomba nijisifu kwamba nimekuwa wako
Wakome wababaifu kunitafuta niliko
Unanipenda kikweli hunifanyii vituko
Pendo lako ni asali wanilisha kwa kijiko
Na wengi hawakubali bado wana babaiko
Niruhusu tafadhali niwapashe yalioko
Nihurumie mwenzako moyo hauna vishindo
Ombi langu liko kwako nisaidie mwenzako
Niachie niwambie kilonigandisha kwako
Alau wazisikie zishe zao chokochoko
Wambea limewasibu hawajuwi tutokapo
Choyo chao kwangu taabu wanidadisi mwenzako
Nakusema sijaribu kilonigandisha kwako
Nangoja yako majibu nipate kibali chakooo
WAKUKUPINGA HAYUPO WALA HATOCHOMOZA
NAOMBA KIBALI CHAKO NIPATE KUWAELEZA
KILONIGANDISHA KWAKO WAO NIKAWAPUUZA