Naomba kuelemishwa kuhusu ulaji wa Samaki wanaofugwa kwenye Mabwawa

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kumekuwa na uwekezaji mkubwa wa ufugaji wa samaki hasa katika Ziwa Victoria.

Hili ni jambo la kupongeza sana na mpaka Wachina wamejenga kiwanda cha vyakula vya hawa samaki.

Juzi nimepita katika eneo la Luchelele Mwanza palipo na mabwawa haya ya kufugia samaki na kushuhudia uvunaji wao.

Wanapovuliwa kwa kweli ni wazima (fresh) kabisa na wanarukaruka jambo lilinipendeza sana lakini cha kushangza rangi yao ni nyeusi tii ukilinganisha na wale wasiofugwa kwenye mabwawa.

Hili la rangi limenipa sintofahamu labda hawa samaki siyo wazuri kwa kuliwa kama chakula.

Ninauliza, Je hawa samaki wa kufugwa ni wazuri kuliwa kama chakula cha binadamu?.

Ninaomba ushauri wa kitalaam.
 
Muulize uyu mtaalamu kwenye huo uzi atakujibu
 
Naomba nikujibu kwa ufupi Mkuu

Hao samaki ni salama kwa matumizi, kuna sababu nyingi zinazopelekea samaki kubalika rangi na kuwa na rangi nyeusi lakini sababu kubwa za kimazingira

Kitaalamu tunaita environmental stress kama vile mabadiliko ya joto, ubora duni wa maji, au kumuexpose kwenye mwanga mwingi/jua

Factors zingine ni kama vile nutritional deficiencies another factor is genetics (nature) kuna species nyingi sana za tilapia na baadhi ya hizo zinakuwa na rangi nyeusi in nature mfano huu hapa kwenye picha
images (3).jpeg
 
Kumekuwa na uwekezaji mkubwa wa ufugaji wa samaki hasa katika Ziwa Victoria.

Hili ni jambo la kupongeza sana na mpaka Wachina wamejenga kiwanda cha vyakula vya hawa samaki.

Juzi nimepita katika eneo la Luchelele Mwanza palipo na mabwawa haya ya kufugia samaki na kushuhudia uvunaji wao.

Wanapovuliwa kwa kweli ni wazima (fresh) kabisa na wanarukaruka jambo lilinipendeza sana lakini cha kushangza rangi yao ni nyeusi tii ukilinganisha na wale wasiofugwa kwenye mabwawa.

Hili la rangi limenipa sintofahamu labda hawa samaki siyo wazuri kwa kuliwa kama chakula.

Ninauliza, Je hawa samaki wa kufugwa ni wazuri kuliwa kama chakula cha binadamu?.

Ninaomba ushauri wa kitalaam.
Kama umezaliwa na kukulia maeneo ya ziwa victoria huwezi shangaa kuona aina hiyo ya sato weusi wakiwa na mistari ya kukatisha. Hiyo ni jamii na ndo walivyo hawa hawakui kufikisha ule unene wa wale wenye rangi ya kungáa
 
Hao na kuku broiler ni sawa tofauti yao huyu ni kuku yule ni samaki
 
Ufugaji wa samaki in it and itself wala hauna shida kwa mlaji iwapo halishwi masumu au kupewa madawa ambayo yana matatizo kwa afya ya mlaji...

Tatizo ni Mazingira na Uwezekano wa magonjwa kwa samaki wengine kwenye ziwa, Sababu unapofuga intensively ni rahisi sana magonjwa kufumuka na yanapofumuka sababu ufugaji ni kwenye cages basi magonjwa hayo ni rahisi kusambaa kwenye ziwa zima hivyo ni hatari kwa kizazi cha samaki...; Hio ndio Risk ya Cage Farming
 
Upate Sato wa maji ya kina kirefu tena wakike anakuwa mtamu balaa achana na hawa wakufunga huwa wana harufu ya vumbi sijui kwanini.
 
Kumekuwa na uwekezaji mkubwa wa ufugaji wa samaki hasa katika Ziwa Victoria.

Hili ni jambo la kupongeza sana na mpaka Wachina wamejenga kiwanda cha vyakula vya hawa samaki.

Juzi nimepita katika eneo la Luchelele Mwanza palipo na mabwawa haya ya kufugia samaki na kushuhudia uvunaji wao.

Wanapovuliwa kwa kweli ni wazima (fresh) kabisa na wanarukaruka jambo lilinipendeza sana lakini cha kushangza rangi yao ni nyeusi tii ukilinganisha na wale wasiofugwa kwenye mabwawa.

Hili la rangi limenipa sintofahamu labda hawa samaki siyo wazuri kwa kuliwa kama chakula.

Ninauliza, Je hawa samaki wa kufugwa ni wazuri kuliwa kama chakula cha binadamu?.

Ninaomba ushauri wa kitalaam.
Najua hawana ladha kama wasiyo wa kufugwa
 
Back
Top Bottom