Naomba kueleweshwa CLEAN SHEET za makipa wa YANGA hesabu zinakataa

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
369
Reaction score
747


Clean sheet inahesabika pale unapotoka na ushindi bila kuruhusu goli
takwimu zinadai kuwa makipa wa Yanga Diarra na Mshery wana Clean sheet 15 na 12
jumla unapata clean sheet 27
hata hivyo Yanga haina Clean sheet 27, Yanga ina clean sheet 22 tu
kuna mechi 8 Yanga imeruhusu magoli
Nakumbuka ni mechi moja tu ndiyo Diarra alidaka nusu na Mshery akaingia Subsitute
nani aniondolee huu utata
NB Mimi ni YANGA KINDAKI NDAKI(SIYO KOLO)

Mechi 8 ambazo Yanga imeruhusu Goli 2021/22
  • Mbeya City 1-1 Young Africans
  • Young Africans 3-1 Ruvu Shooting
  • Namungo 1-1 Young Africans
  • Tanzania Prisons 1-2 Young Africans
  • Biashara United 1-1 Young Africans
  • Azam 1-2 Young Africans
  • Young Africans 2-1 Biashara United
  • Young Africans 2-1 Namungo
Clean sheets 22 za Yanga 2021/22
  • Kagera Sugar 0-1 Young Africans
  • Young Africans 1-0 Geita Gold
  • KMC 0-2 Young Africans
  • Young Africans 2-0 Azam
  • Mbeya Kwanza 0-2 Young Africans
  • Simba 0-0 Young Africans
  • Young Africans 4-0 Dodoma
  • Coastal Union 0-2 Young Africans
  • Polisi Tanzania 0-1 Young Africans
  • Young Africans 0-0 Mbeya City
  • Mtibwa Sugar 0-2 Young Africans
  • Young Africans 3-0 Kagera Sugar
  • Geita Gold 0-1 Young Africans
  • Young Africans 2-0 KMC
  • Young Africans 0-0 Simba
  • Ruvu Shooting 0-0 Young Africans
  • Young Africans 0-0 Tanzania Prisons
  • Dodoma 0-2 Young Africans
  • Young Africans 4-0 Mbeya Kwanza
  • Young Africans 3-0 Coastal Union
  • Young Africans 2-0 Polisi Tanzania
  • Young Africans 1-0 Mtibwa Sugar
 
Utaelewa tu mkuu muda ukifika. Kwa sasa endelea tu kuvumilia. Msimu huu Tanzania One katuangusha kabisa, kiasi cha kuachwa benchi na kocha wake kwenye mechi mbili za mwisho za ligi.

Wale wenzangu na mimi waliokuwa wakimkejeli Diarra aliposajiliwa, kwa sasa aibu tu ndiyo imewajaa.
 
Naona baada ya Manure kupigwa K. O kwenye cleansheat umeanza hesabu zako za Magazijuto hapa. Na utaumia sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa mahesabu hayo, inawezekana hata Kabwili akawa na clean sheet nyingi maana hakufungwa
 
Msheri alikuja Yanga katikati ya masimu akitokea Mtibwa. Hivyo kwa kuwa ligi ni moja alikuja na cleansheet zake kutoka mtibwa akaendeleza Yanga. Sio kwamba zote kazipatia Yanga.
Ni sawa ma mchezaji abadili timu katikati ya msimu mabao yatajumlishwa kwa timu zote alizocheza kwa msimu husika.
 
Kuna watanzania ni wapuuzi sana, badala ya kujibu hoja wao wamekazana kumkejeli mtoa mada.

Kama hamna majibu sahihi mngepita tu kimya kimya kama ambavyo mimi sina jibu na bila huo ujinga wenu ningepita kimya kimya.
 
Naam inaweza kuwa ni kweli, maana kwa namna msheri alivyokaa bench asingefikisha hizo 12 na diara 15
 
Mjadala umeishia hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…