Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,674
- 2,470
Ili kuelewa vyema hili suala ni vizuri kufahamu presha.
A: Presha ni nini?
Msukumo wa kimiminika cha damu kwenye ukuta wa mshipa/mishipa ya damu.
B: Aina mbili za upimaji wa presha
Presha hupimwa kwa vipimo viwili:
1: Systolic (S)/presha inayoandikwa juu: ni ile ambayo hupimwa wakati moyo unasukuma damu kwenda mwilini(kumbuka moyo ni pumpu).
2: Diastolic (D)/presha inayoandikwa chini: ni prrsha inayopimwa wakati moyo unafunguka ili kupokea damu toka mwilini.
B: Kiasi/kiwango cha presha na mgawanyo wake
1: Presha ya kawaida/normal: S < 120 mmHg na D < 80 mmHg
2: Iliyopanda/eleveted: S=120-129 mmHg na D= < 80 mmHg
3: Tatizo la presha daraja la kwanza: S=130-139 mmHg au D=80-89 mmHg
4: Tatizo la presha daraja la pili: S=140 mmHg/zaidi au 90 mmHg/zaidi.
5: Tatizo la presha daraja la tatu: S >180 mmHg na/au D >120 mmHg (huitaji tiba ya dharura/haraka).
NB: Presha namba 1 ni kawaida.
Presha namba 2-3 na sehemu ya 4 huweza kuwekwa sawa kwa kubadili na kusimamia mwenendo mwema wa maisha ya mtu juu ya kuzuia viwezeshaji/risk factors. Ingawa kwa ushahidi uliopo, presha namba tatu huitaji matumizi ya dawa ili kuzuia madhara yatokanayo na kuoanda kwake wakati huo ukifanya mabadiliko chanya kwenye maisha. Marekebisho hayo yana ushahidi wa kisayansi kuweza kurejesha presha kuwa sawa. Hii huusisha:
1: Matumizi kidogo ya chumvi
2: Kupunguza uzito
3: Kufanya mazoezi/aerobic.
4: Matumizi sahihi ya pombe
5: Kusitisha uvutaji sigara
6: Kupunguza matumizi ya wanga
7: Kuhakikisha kuwa na uwiano mzuri wa mafuta/cholesterol.
Kwa presha iliyofika kwenye daraja la tatu, pamoja na kuhitaji mabadiliko ya kimaisha, bado huitaji matumizi ya dawa kwa kipindi chote cha maisha ya mhusika. Hii hutokana na:
1: Presha hii haitaondoka yote, hata ukizingatia mwenendo mwema wa kimaisha.
2: Presha hii ni kiasi ambacho kitaleta madhara kwenye viungo vya mwili kama: moyo, figo, macho, ini, mishipa ya damu, ubongo nk.
3: Taarifa halisi ya nini kifanyike, hutegemea na mgonjwa husika, tathmini ya viwezeshaji presha/risk factors, kiasi cha presha na malengo wakati wa tiba.

Habari zenu nategemea mpo salama naomba kueleweshwa kitu
Hivi unaweza kutumia dawa za presha na ukakaa sawa?
Namaanisha unaweza kutumia dawa bila kuacha na maisha yakaendelea kama kawaida?