Foundation Programme (OFP) ni kozi ya maandalizi kwa wanafunzi wa makundi matatu.
1. Waliomaliza form 6 na hawakupata principal pass mbili zenye cutoff point ya 4. Ila wanaopaswa kuwa na walau principal pass moja na subsidiary moja (1.5 cutoff point)
2. Waliomaliza Diploma lakini hawajafikisha GPA ya 3.0 ila wawe na GPA inayoanzia 2.0.
3. Wanaohama profession moja kwenda nyingine. Mfano umesoma Diploma ya Education then unataka kusoma Bachelor ya Law ni profession mbili tofauti kabisa hivyo utapaswa kusoma kwanza Foundation Programme.
Mpaka mwaka 2016 vyuo karibu vyote vilikua na Foundation programme lakini ilifutwa na ikarudishwa mwaka 2018 ikiwa na vigezo tofauti kama nilivyoainisha hapo juu na Chuo Kikuu Huria kikapewa jukumu la kutoa programme hiyo ya Foundation.