Kifupi mkuu Qatar mara kwa mara inakuwa nchi tajiri zaidi duniani kwa pato la mtu mmoja mmoja. Wana mafuta mengi na Gas nyingi sana.
Pamoja na utajiri wao huo wana eneo dogo sana nchi yao ni kilomita za mraba kama 11,000 tu, kujua ni ndogo kiasi gani Tanzania Nzima ina kilomita za mraba zaidi ya 900,000
Hii ramani ya dunia ikionesha Qatar
View attachment 2172395
Vitu maarufu vya Qatar kabla ya world cup ni Kituo cha Tv Aljazeera, Club ya PSG pengine na Qatar Airways.
Hili ndo jiji lao la Doha.
View attachment 2172401
Jambo muhimu la kufahamu kwa Mtanzania kuhusu hii world cup ni kwamba hawa jamaa wapo wachache sana, kiasi kwamba hata wachezaji wa world cup hakuna, hivyo muda mrefu sana walikuwa wakitafuta mamluki. Kuna waTanzania wengi wameenda, Tetesi watoto wa Kibadeni wapo huko na Hata mshambuliaji wao mmoja Akram Afif ni Mtu wa Qatar mwenye asili ya Tanzania. Pia wachezaji wao wengi wametoka Africa sehemu kama Senegal, Sudan etc.
Hichi kikosi chao
View attachment 2172403
Pia kutokana na udogo wa eneo viwanja vya mpira na miundombinu mengine wamejenga tu kwa muda world cup ikiisha wanabomoa na watavitoa misaada kwa Nchi nyengine.