1: Kuondolewa kizazi kwa sababu ya uvimbe, maana yake uvimbe umeonekana kuleta madhira. Na kwa kiasi chake ingawa haujakionyesha au kwa vigezo vingine pia, daktari ameona ni vyema kuondoa vyote.
2: Suala la kukutana kinyumba. Mji wa uzazi hauusiki kabisa. Kwani hili hufanyika ndani ya njia (pipe) inayoelekea kwenye mji wa mimba/vagina. Ni mara chache ambapo baba huweza kugusa tu mlango wa mji wa mimba na si kuingia ndani. Hivyo, haitakuwa na mabadiliko yoyote.