Naomba kufahamishwa juu ya sheria ya head to head

Naomba kufahamishwa juu ya sheria ya head to head

Mbona rahisi tu, mfano kwa mashindano ya CAF head to head ni kanuni inayofuata baada ya points. Lakini kuna kanuni zingine baada ya points na head to head. Maana yake kama points na head to head wanalingana wanaenda kwenye kanuni nyingine kama vile GD na yenyewe kama wanalingana wanaangalia magoli mengi ya kufunga au kufungwa n.k

Pia kumbuka mashindano mengine kanuni ya kwanza ni points halafu inafuata GD halafu head to head n.k
 
Wanaangalia matokeo mlivyokutana home and away. Kuna mmoja atakua kapelea tu kwa mwenzie
Shida ni kwamba timu A anaweza akawa na advantage ya H2H kimagoli dhidi ya timu B lakini akakosa advantage hiyo mbele ya timu C, na timu C naye ambaye ana advantage ya h2h mbele ya timu A akakosa advantage ya h2h kimagoli dhidi ya timu B.
 
Kwanini unarudia rudia kwamba timu zote A, B na C zina pointi 10.

Maana hii kila mtu anajua ndio maana umekuja swali la kwamba je, tunapataje wawili kati ya hao watatu wenye pointi 10, kwa kutumia H2H.

Sasa kwenye head to head utaratibu ni kwamba hao wenye pointi 10, yanaangaliwa matokeo ya walivyocheza wao kwa wao (mechi zote zilizowahusisha "wenyewe").
Yaani
A vs B,
Bvs A
A vs C,
C vs A
B vs C
C vs B

Matokeo hayo yanatengenezewa msimamo.
Kwenye huo msimamo ndipo kwa matokeo yako uliyoyaleta katika uzi ni kwamba:
A anakua na pointi 7,
C anakua na pointi 6
B anakua na pointi 4

Hivyo basi kwa matokeo ya head to head (kati ya A, B na C) ni kwamba A anatakiwa kuwa juu, anafuatiwa na C na kisha B anafuata. Lakini kwenye msimamo mkuu hawa wote wana pointi 10.

Kundi litakua hivi:
1. A pt 10
2. C pt 10
3. B pt 10
4. D pt .....

Wawili watakao songa mbele ni A na C kwa sababu ya matokeo yao mazuri kwenye ule msimamo wa "Head to Head".

Usipoelewa hapa, naleta wazungu.

Google sentensi hii

How does head to head break a tie of three teams
Kiongozi asante sana ubarikiwe nimeelewa. Kumbe zile jumla ya point zilizovunwa zinawekwa kando. Zinahesabiwa zilizovunwa mlipokutana timu tatu zilizofungamana. Shukrani sana
 
Je kwa matokeo ya aina hiyo juu timu ipi ambayo inatolewa kwa sheria ya head to head kati ya timu hizo tatu?
Msimamo utakuwa hivi:
1647697715827.png

NB: Timu A na C zimelingana points. Kwa kuwa umezungumzia kanuni ya Head to Head, zilipokutana nyumbani kwa C matokeo yalikuwa 3-1, na zilipokutana nyumbani kwa A matokeo yakawa 2-0. Kwa kuwa zote lililingana points 3, kanuni ya Head to Head inaipa faida timu A kwa kuwa ilipata magoli mengi zaidi ugenini (goli 1) kulinganisha na timu C
 
Hapo kiongozi sijakumanya
Mmmmmmmh.... Itakua kazi kuelewa

Head to head inahusisha timu zilizolingana alama. Kwenye mfano timu zilizolingana pointi ni A, B, na C.
Kwahiyo head to head itazohusisha hizo.

Itazihusisha vipi, ni kwa kuangalia matokea ya walipokutana wao kwa wao. (Ligi ya watatu yaani A, B na C)

Matokeo umeyaleta mwenyewe...
Tumekupangia msimamo wa H2H.
Kapatikana anayekaa juu, na chini.

Unasema sisi hatujakuelewa na tumemsahau timu D.

Sasa kama hili tu haulielewi, sasa si tutajaza seva za Maxence Melo ndugu yangu.

Au basi.

Watarusha shilingi juu.
 
Msimamo utakuwa hivi:
View attachment 2156872
NB: Timu A na C zimelingana points. Kwa kuwa umezungumzia kanuni ya Head to Head, zilipokutana nyumbani kwa C matokeo yalikuwa 3-1, na zilipokutana nyumbani kwa A matokeo yakawa 2-0. Kwa kuwa zote lililingana points 3, kanuni ya Head to Head inaipa faida timu A kwa kuwa ilipata magoli mengi zaidi ugenini (goli 1) kulinganisha na timu C
B ameshinda mech tatu katoa sare moja hivyo ana point kumi pia
 
Kiongozi asante sana ubarikiwe nimeelewa. Kumbe zile jumla ya point zilizovunwa zinawekwa kando. Zinahesabiwa zilizovunwa mlipokutana timu tatu zilizofungamana. Shukrani sana
Kuangalia goal difference za jumla ni kigezo ambacho sio fair na ndio maana la Liga na CAF huwa wanatumia Head to Head kama first tie breaker.

Kivipi ?

Ni hivi;
Kama Simba na Asec wamefanana pointi, na anatakiwa mmoja kati yao, basi zichukuliwe mechi baina ya wawili haohao (bila kumhusisha Berkane na USGN).

It is very unfair kuchukua matokeo ya Simba vs Gendamerie yatumike kuamua mbabe kati ya Simba na Asec.
Wamalizane wao wenyewe. Na hii ndio maana ya head to head.

Hivyo basi, head to head inaweza kuamua timu mbili zilizofanana, timu tatu, nne, saba hata tisa.
Cha msingi tu, yatapambanishwa matokeo ya wote wanaohusika na mfanano, na kuyaondoa matokeo ya wote wasiokuwepo kwenye huo mgogoro.
 
Mmmmmmmh.... Itakua kazi kuelewa

Head to head inahusisha timu zilizolingana alama. Kwenye mfano timu zilizolingana pointi ni A, B, na C.
Kwahiyo head to head itazohusisha hizo.

Itazihusisha vipi, ni kwa kuangalia matokea ya walipokutana wao kwa wao. (Ligi ya watatu yaani A, B na C)

Matokeo umeyaleta mwenyewe...
Tumekupangia msimamo wa H2H.
Kapatikana anayekaa juu, na chini.

Unasema sisi hatujakuelewa na tumemsahau timu D.

Sasa kama hili tu haulielewi, sasa si tutajaza seva za Maxence Melo ndugu yangu.

Au basi.

Watarusha shilingi juu.

Mkuu ulishanuelewa kwenye post namba 20 nami kwenye post 23 nimekili kuwa nimekuelewa.
IMG_20220319_170320.jpg
 
B ameshinda mech tatu katoa sare moja hivyo ana point kumi pia
Hapana, angalia vizuri. B ameshinda tatu zote za nyumbani na ugenini 0-1 dhidi ya D. Hizo ni point 12, sio 10
 
Shida ni kwamba timu A anaweza akawa na advantage ya H2H kimagoli dhidi ya timu B lakini akakosa advantage hiyo mbele ya timu C, na timu C naye ambaye ana advantage ya h2h mbele ya timu A akakosa advantage ya h2h kimagoli dhidi ya timu B.
Mbona u mgumu kuelewa? head to head ni kama vile points tu. Kwamba mwenye points nyingi ndie atasonga mbele na kama points wana fanana basi watangalia head to head kwa maana nani kamfunga mwenzie na kamfunga magoli mangapi.
Kama hivyo vyote wanafanana wataangalia GD na kama wanafanana pia wataaangalia kati ya wote nani ana magoli mengi ya kufunga kwa ujumla pia kama wanafanana wataangalia yupi kafungwa magoli machache n.k

Kanuni zipo nyingi ya kuamua yupi asonge na ya kwanza kabisa ni points inayofuata inategemeana na mashindano , inaweza ikawa head to head au GD n.k
 
Kuangalia goal difference za jumla ni kigezo ambacho sio fair na ndio maana la Liga na CAF huwa wanatumia Head to Head kama first tie breaker.

Kivipi ?

Ni hivi;
Kama Simba na Asec wamefanana pointi, na anatakiwa mmoja kati yao, basi zichukuliwe mechi baina ya wawili haohao (bila kumhusisha Berkane na USGN).

It is very unfair kuchukua matokeo ya Simba vs Gendamerie yatumike kuamua mbabe kati ya Simba na Asec.
Wamalizane wao wenyewe. Na hii ndio maana ya head to head.

Hivyo basi, head to head inaweza kuamua timu mbili zilizofanana, timu tatu, nne, saba hata tisa.
Cha msingi tu, yatapambanishwa matokeo ya wote wanaohusika na mfanano, na kuyaondoa matokeo ya wote wasiokuwepo kwenye huo mgogoro.
Ni pia Uefa champions league, na Seria A wanatumia head to head
 
Huu uzi una husiana nini na habari ya Simba? Wabongo aisee tunasafari ndefu sana juu ya akili za usimba na uyanga. Utafikiri watu wamelogezewa na hizi timu za kariakoo kiasi kwamba mawazo yamebakia kwenye uyanga na usimba hata kwa vitu visivyo husiana. Ni aina ya ulevi huu
Sasa hapo unahusisha uyanga nani kaongelea Yanga. Mimi nimekwambia subiri April 3 utaona mfamo wa simba akivuka ndio utapata majibu
 
Sasa hapo unahusisha uyanga nani kaongelea Yanga. Mimi nimekwambia subiri April 3 utaona mfamo wa simba akivuka ndio utapata majibu
Simba inafika vipi kwenye sheria ya head to head? Maana swala la Simba na hii mada mbona haihusiani.
 
Timu A na Timu C zitasonga hatua inayofuata kwakuwa wana idadi kubwa ya magoli lakin point naona kama zimelingana kwa Timu A B na C
Hivyo goal difference lazma itazingatiwa hapo kupata nani wa kuendelea na stage inayofuata..
 
Isikupe shida Simba tunatakiwa kushinda berkane wanamagori mengi sanaa nawao wafungwe ujinga huu tumejitakia
 
Back
Top Bottom