Naomba kufahamishwa kampuni nzuri ya bima za Magari ambao siyo wasumbufu

Wakuu naombeni ushauri. Nilikatia gari yangu bima premium ya 8milion. Bahati mbaya gari ikapata ajali na haitengenezeki so bima wakatakiwa kunilipa. Katika offer waliyonipa wanasema pre accident value ni 5.5milion. Nisichoelewa ni kwa nini wanikatie bima ya 8m ikiwa wanajua value ya gari yangu ni 5.5milion. Naombeni ufafanuzi kwa hili maana hata emails zangu sasa hawajibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana kabisa ikawa ni kweli thamani ya gari lako kipindi linapata ajali ilikua ni 5.5m tatizo ni pale mwanzo saa unakata bima ulipaswa kulikatia kwa market value labda ingekuwa 6m..

Hapo ndio bima wanapoenekana ni wababaishaji hawakuelezi vizuri wenyewe wanataka pesa tu..

Mara zote kinachoshusha thamani ya gari ni uchakavu (depreciation) hapo wanaangalia kuanzia lini gari lako limesajiliwa hapa nchini.. kama lina muda mrefu ndio inakula kwako unajikuta bora ungekata bima ndogo tu..

Next time kabla ujakata bima fanya valuation ya gari lako kwa bei ya soko kwa wakati huo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na je ni kwa nini waliendelea kupokea premium ya 8m na si value waliyoithaminisha. Maana kila ninapolipa wanaipiga picha gari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naombeni ushauri. Nilikatia gari yangu bima premium ya 8milion. Bahati mbaya gari ikapata ajali na haitengenezeki so bima wakatakiwa kunilipa. Katika offer waliyonipa wanasema pre accident value ni 5.5milion. Nisichoelewa ni kwa nini wanikatie bima ya 8m ikiwa wanajua value ya gari yangu ni 5.5milion. Naombeni ufafanuzi kwa hili maana hata emails zangu sasa hawajibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mchezo alikuchezea huyo aliyekukatia. Meaning nikuwa ameivalue gari yako kuwa ni ina thamani hiyo waliyokupa ambayo ni tofauti na price ya uthaminishaji halisi. At least angekuelewesha kwanza na mkubaliane ili nyote muwe on the safe side. Sasa hapo tafasiri yake ni kuwa jamaa amekupiga changa la macho na inabidi ulie na huyo agent maana ndiye kakuchezea rafu.
 
Mtego ni kwamba wewe mteja mwenye gari ndio unapaswa kusema bei ya gari lako, ungekutana na muungwana angekueleza faida na hasara za kujipangia thamani ya gari lako..

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu atakuwa alikuwa anapigwa hiyo chenji ya bei ya gari baada ya kutoa hicho kiasi.
 
Kuna mchezo alikuchezea huyo aliyekukatia. Meaning nikuwa ameivalue gari yako kuwa ni ina thamani hiyo waliyokupa ambayo ni tofauti na price ya uthaminishaji halisi. At least angekuelewesha kwanza na mkubaliane ili nyote muwe on the safe side. Sasa hapo tafasiri yake ni kuwa jamaa amekupiga changa la macho na inabidi ulie na huyo agent maana ndiye kakuchezea rafu.
Inatakiwa kuwa na thamani halisi wakati wa kukata bima unashauriwa kutumia valuers ili wakutajie thamani halisi. Gari mnaweza ukanunua pamoja kila mtu na lake kwa miaka 4 yakipata ajali yanaweza yakalipwa tofauti kwa sababu mbalimbali. Mfano gari ya kwanza ameiongeza thamani kwa kubadilisha baadhi ya vitu (sio matairi) thamani yakse hubadilika ila gari ya pili gari haijaongezwa chochote thamani yake hushuka.

Nchi jirani wenzetu hushauriwa kwenda na ripoti ya valuers kwenda kukata bima ili kupata thamani halisi ya bima.

Pia kuna kundi ambalo hukata bima ndogo kuliko thamani yake nao hukumbana na matatizo yao.

Ushairi wangu kata bima kwa kutumia thamni halisi na si vinginevyo,kwani kazi ya bima ni kukurudisha pale ulipo kabla ya kupata ajali(hii ni kwa bima za ajali ambazo sio bima za maisha)
 
Inawezekana kabisa ikawa ni kweli thamani ya gari lako kipindi linapata ajali ilikua ni 5.5m tatizo ni pale mwanzo saa unakata bima ulipaswa kulikatia kwa market value labda ingekuwa 6m..

Hapo ndio bima wanapoenekana ni wababaishaji hawakuelezi vizuri wenyewe wanataka pesa tu..

Mara zote kinachoshusha thamani ya gari ni uchakavu (depreciation) hapo wanaangalia kuanzia lini gari lako limesajiliwa hapa nchini.. kama lina muda mrefu ndio inakula kwako unajikuta bora ungekata bima ndogo tu..

Next time kabla ujakata bima fanya valuation ya gari lako kwa bei ya soko kwa wakati huo..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii unaifanyaje?
 
Back
Top Bottom