Naomba kufahamishwa kiwango cha elimu ya Rais Samia Suluhu Hassan

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
379
Reaction score
466
Kwa wajuzi naomba kujua kiwango cha elimu Cha Rais wetu wa sasa mama Samia Suluhu Hassan na pia kujua viwango vya elimu vya Marais watano waliopita na siyo vibaya tukaujua ni Rais yupi alikuwa na elimu kubwa zaidi na Rais yupi alikuwa na elimu ndogo. Lengo ni kufahamu wasifu na historia za viongozi wetu wakuu wa nchi.

Lakini pia naomba kujuzwa katika Katiba kuna kipengele kinachozungumzia suala la kiwango cha elimu anachopaswa kuwa nacho Rais wa nchi au halijatajwa hilo.

Je, kiwango cha elimu kina athari gani kwa uongozi mkubwa kabisa katika nchi? Hili ningependa nijulishwe na wabobezi wa siasa.
 
Wewe siku zote hizo walikuwa wanasoma wasifa wake kwenye channels kibao za Tz hukusikiliza?
 
Mnataka kujua elimu ya Rais kwani mnataka kutambika?
Muhimu kujua,taasisi hii muhimu isipo wekea taratibu makhususi kila mtu ataamini anaweza kuwa rais na tutakuja kupata Marais wa hovyo Sana mbeleni Kama dalili zinavyoanza kuonekana kwa hiyo kunaumuhimu wa kuanza kuulizana .
Lugha pekee Yani kutema yai haiwezi kuwa kigezo Cha elimu tunahitaj kujua pengine itatusadia kujua tupo na viongozi wa aina gani.
 
Wasifu wake ulielezwa sana baada ya yeye kuapishwa mkuu kwamba hakuna sehemu hata moja ulipofanikiwa kusikia au kusoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…