Naomba kufahamishwa kuhusu bachelor degree ya Education in Earlychildhood

De panther

Member
Joined
Jul 9, 2022
Posts
80
Reaction score
108
Habari za muda huu wanajamvi.

Naomba kufahamu zaidi kuhusu elimu tajwa hapo juu.

Mimi ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2022,nimesoma tahasusi ya HKL.

Hivyo naomba mwenye ufahamu anipe dondoo kuhusu elimu hii.

Ahsanteni.
 
Achana na kazi ya kufundisha wanaadamu, siku hizi mwalim ni pesa na muda. Acha kusoma nenda kijijini kwenu kata eneo lima
 
Ushauri pekee ambao ni muhimu ni kwamba achana na kozi za education, ukishindwa kabisakabisa labda ile yenye special needs education au physical education...

ILA ACHANA NA HABARI ZA KOZI ZA UALIMU maana utakuja kumpa Mungu lawama za bure kukuumba mwanadamu
 
Ahahah!! Sawa mkuu nimekupata
 
Habari za muda huu wanajamvi.
Naomba kufahamu zaidi kuhusu elimu tajwa hapo juu.
Mimi ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2022,nimesoma tahasusi ya hkl.
Hivyo naomba mwenye ufahamu anipe dondoo kuhusu elimu hii.
Ahsanteni!!!
Soma hiyo mkuu, kama n Education kwa Arts subject hyo ndo ya kusoma lazma watakuajili tu ajira za ualimu mwaka huu wengi wamechukuliwa ndo wanafit zaidi kufundisha primary school
 
Ukifika chuo soma English language usiende soma sjui ma KI sjui Ma KF (Na maanisha kiswahili)
 
Wewe soma tu..ila usjie humu kulialia kusema serikali inaajiri lini?

Mana walimu mnatusumbua sana kwa nyuzi za kulialia..mnakera sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa anaeenda kusoma Ualimu wa Science hakikisha unasoma Physics aisee na ukapata ka G.P.A kazuri basi wewe kitu kinaitwa tatzo la ajira utaliskia kwa majilani tu, maana Physics mwenye G.P.A nzuri huwezi kaa mtaani miaka mitatu hujaajiliwa sio ukasome Biology basi utaishi kwa kuomba maajaliwa
 
Wewe soma tu..ila usjie humu kulialia kusema serikali inaajiri lini?

Mana walimu mnatusumbua sana kwa nyuzi za kulialia..mnakera sana.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu akisoma hyo education ya Early childhood na akasoma English hawez kuja tusumbua sababu serikali inawajili hao kuwapeleka primary kwa wingi ata private schools level ya primary hawezi kosa kazi
 
Habari za muda huu wanajamvi.
Naomba kufahamu zaidi kuhusu elimu tajwa hapo juu.
Mimi ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2022,nimesoma tahasusi ya hkl.
Hivyo naomba mwenye ufahamu anipe dondoo kuhusu elimu hii.
Ahsanteni!!!
Ni course ya ualimu wa shule ya msingi; kwa ajira za juzi hapa walipendelewa sana waliosoma hiyo degree; ingawa sikushauri sana uisome
 
Habari za muda huu wanajamvi.

Naomba kufahamu zaidi kuhusu elimu tajwa hapo juu.

Mimi ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2022,nimesoma tahasusi ya HKL.

Hivyo naomba mwenye ufahamu anipe dondoo kuhusu elimu hii.

Ahsanteni.
Ni moja ya kozi ambayo ni nzuri lakini pia ina fursa nyingi mbali na kuwa mwalimu na usikatishwe tamaa na mtu kikubwa angalia nn kinafaa binafsi nakusihi uende ikiwezekana nenda udsm au makumila ipo arusha.
 
Nashukuru mkuu....naona hapa una madini ya kutosha,naomba nisaidie namba yako ya whatsap kama hutojali.
 
Back
Top Bottom