Naomba kufahamishwa kuhusu tabia hii ya kuku

Naomba kufahamishwa kuhusu tabia hii ya kuku

Plutoz

Member
Joined
May 13, 2015
Posts
18
Reaction score
6
Naomba kufahamishwa kuhusu tabia hii ya kuku wa kienyeji
Nina kuku wangu wa kienyeji pure ametaga kafikisha mayai 10 na ndio mtago wake wa kwanza lakin ameanza tabia ambayo sijaielewa ikifika jion anaenda kwenye kiota chake cha mayai analalia ikifika asubui wakati nafungua banda anatoka na harud tena kulalia mpaka ikifika jion muda wa kuingia bandani na leo ni siku ya pili kafanya hivyo :
1.sasa nilitaka kujua ndio inavyokuwa kwa kuku anaeanza kulalia/kuatamia kufanya hivi kwa siku za kwanza au sio mlaliaji mzuri
2.je mayai yatakua salama kwa style hii aliyoifanya kulalia usiku tu kwa siku mbili
3.je nifanye nini kuyaokoa mayai yasiharibike kama itakua bado hayajaharibika?
 
Jaribu kwenda kwa mtaalam wa mifugo ukapate ushauri
 
Huyo kuku tunamuita mvia(sawa na mtu asietaka kufanya kazi) mchinje haraka na mayai leta hapa
 
Labda sio kuku wa kienyeji asilimia mia. Hybrid kienyeji wengine huwa hawatamii na wenye kuku hao utumia incubator kuangua mayai
 
Cha kufanya ni, anapokwenda kulalia jioni/usiku nenda kamchikoze, fanya kama unamtoa. Kwa kuku ambaye amemaliza kutaga na anaatamia kuna sauti ataitoa (sauti ya kuatamia). Kama atafanya hivyo jua kwamba anaatamia, na kama anaatamia kwa mtindo huo jua hawezi kuatamia na ataharibu mayai. Kwahiyo hayo mayai yatumie kwa matumizi mengine, kama kula ama kumpa mwingine aatamie.

Kama hatoi sauti ya kuatamia basi jua anaweza akayaaribu mayai. Kwahiyo hayo mayai yatoe kwenye kwenye kiota umbakizie 3 ili asibadili mahali pa kutaga. Itakapofika siku ya kuatamia, muwekee hayo mayai hasa usiku wanapoingia kulala
 
Huwa inatokea kwa siku za mwanzo mkuu, baada ya siku chache hukaa moja kwa moja
huku akitoka mara moja moja.
 
Naomba kufahamishwa kuhusu tabia hii ya kuku wa kienyeji
Nina kuku wangu wa kienyeji pure ametaga kafikisha mayai 10 na ndio mtago wake wa kwanza lakin ameanza tabia ambayo sijaielewa ikifika jion anaenda kwenye kiota chake cha mayai analalia ikifika asubui wakati nafungua banda anatoka na harud tena kulalia mpaka ikifika jion muda wa kuingia bandani na leo ni siku ya pili kafanya hivyo :
1.sasa nilitaka kujua ndio inavyokuwa kwa kuku anaeanza kulalia/kuatamia kufanya hivi kwa siku za kwanza au sio mlaliaji mzuri
2.je mayai yatakua salama kwa style hii aliyoifanya kulalia usiku tu kwa siku mbili
3.je nifanye nini kuyaokoa mayai yasiharibike kama itakua bado hayajaharibika?

Jamani asanteni sana kwa mchango wenu ila nimejifunza kua hii ni moja ya tabia ya kuku mwanzo anakua anasuasua ila baadae analalia vizuri tu,maana tarehe 20 july 2017 alitotoa mayai yake yote 11 na hakuna lililoharibika wala aliloacha kutotoa
 
Huwa inatokea kwa siku za mwanzo mkuu, baada ya siku chache hukaa moja kwa moja
huku akitoka mara moja moja.

Nimekukubali uliyosema ndio nimeyaona asante sana kwa kunifahamisha mkuu kuku wangu katotoa mayai yake yote 11 na hajaacha hata moja
 
Ni huyu hapa
4e7c4f1ce2890e5170a31a69a64cd1d7.jpg
2a7851a4269c230d08060c378af627eb.jpg
24983998018a92369a3b7ece04941d71.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tunamuepusha na kunguru mkuu na usumbufu
Kweli kabisa kaka kunguru waharibifu sana!nigawi kifaranga na mm nifuge mkuu wangu

Sent from my TV
 
Back
Top Bottom