Gari inategemea na unapenda nini.
Unaponunua gari kama brevis, mark X, GX 110 , Lexus GS, LS na gari zinazofanana na hizo ambazo injini zake CC inaanzaia 2500 plus
Kuna faida kadhaa utapata
1. Luxury - gari hizo zote zina comfort, Safety ya juu kama ukipata ajali.
2. Injini ina power kubwa, sio tu ya ku overtake na kukimbia, lakini gari inakuwa stable barabarani, gari inatulia na nzito. Inakuwa inamudu barabara complex kidogo, milima nk nk
Tatizo ni moja tu na si tatizo la gari husika ni Tatizo la Masikini sisi. (limited financial)
-Gari inakuwa na unywaji wa mafuta wa juu kidogo kulinganisha na gari ndogo kama Vitz, IST, Porte nk
Sasa hivi Vigari vinavyokunywa Mafuta vizuri. Raha yake na faida ni hapo tu kwenye Mafuta. Hususani ukiwa huna uchumi mzuri lakini Pia pengine ni Cheap kufanya Mantainance /Service.
Lakini hizi gari ndogo Vitz, Porte, IST na ndugu zao wote. Unakosa vitu kadhaa
1. Havina comfort. Sio luxury ni sawa na kulalia Godoro la bei nafuu kabisa linaloumiza mgongo wakati mwenzio analalia Tanform Arusha tena ya Spring
2. Hazina power ya kutosha, kuhimili complex roads, unaweza ingia hata kwenye tope dogo tu usitoke. Lakini hazitulii barabarani kulinganisha na hizo za injini kubwa.
3. Safety yake ni ndogo, ukipata ajali unakunjwa kama karatasi lakini mifumo mingine pia ya kiulinzi inakuwa sio advanced
Mwisho wa siku ni uchaguzi wa mnunuzi nini unataka. Kutokana na gari husika.
Huwezi kulinganisha Raha ya Crown dhidi ya Raum
Kazi ni kwako binafsi bora nipambane na mafuta ila niwe Comfortable