Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Naomba kufahamishwa kwa kina kuhusu picha maarufu ya Monalisa

Hakuna mwenye maana kamili juu ya hiyo picha. Ila tuu, mambo mengi yaliyomo katika hiyo picha ni kama baadhi ya wadau walivyotangulia kusema hapo kabla. Ngoja nikupe summary ya baadhi.

1. Picha inabadilikabadilika face impression yakeukiiangalia tokea angle tofautitofauti.

2. Kuna wanaoona kuwa kuna alama za secret societies kama Freemason, skull and bones ndani ya hiyo picha.

3. Kuna wanaoona kuwa hiyo sura ni mjumuisho wa sura mbili kati ya mwanamke na mwanamme.

Bonus :

Ni miongoni mwa picha aghali katika kipindi chake. Kwani Miaka ya 1500, mfalme Francis I wa ufaransa aliinunua picha hiyo kwa kilo 13 za dhahabu ambayo kwa leo ni sawa na dola laki sita na nusu za kimarekani.
mamaeee "" kwa sasa si " 2billions hiyo
 
ukiiangalia kuna muda inahuzuni kuna muda inafuraha
 
Mwenye hiki kitabu cha leonardo kinaitwa the "angels and demons" pamoja na"fortress" naomba aviweke hapa kwani ni msaada tosha wa yote tunayo ya jadili mahala hapa
 
Dah mkuu una macho mangapi mbona mimi naona sura moja tu
watu wanacomplicate tu da vinci amechora simple kama arts nyengine ila kwa kuwa kachora genious basi ndo imekuwa kiki ya enzi.
 
Itizame hapo. Inasemekana Leonardo Da Vinci alijichora kwa muktadha wa kama angezaliwa mwanamke angekuwa na muonekano gani- uzuri na kila aina ya sifa ya mwanamke.

Ukiitizama hiyo picha kwa umakini utagundua kwamba inakutazama kwa kila angle utakayokuwa(perception) na mambo chungu nzima like secret codes na kadhalika
tapatalk_1530705276453.jpeg
 
Habari ya muda huu wanajanvi!

Rejea mada inavyojieleza hapo juu,
Mchoro wa Monalisa ni moja kati ya michoro mingi duniani ulioweza kuchorwa na mwanasayansi na mchoraji Leonardo da Vinci mnamo karine ya kumi na sita(16).

Mchoro wa Monalisa ulianza kujipatia umaarufu baada ya kuibiwa mwaka 1911 kutoka katika makumbusho ya Louvre, mjini Paris Ufaransa.

Baada ya kuibiwa kwa mchoro wa Monalisa watu wengi mashuhuri katika sanaa walianza kutunga nyimbo na mashairi yaliyohusiana na upotevu wa mchoro wa Monalisa. Jambo lililopelekea kukua kwa umaarufu wa Monalisa.

Lakini ukweli ni kuwa mchoro wa Monalisa umepata umaarufu kwa "kutokua na maana yoyote"


MAONI YANGU JUU YA

PICHA YA MONALISA:

1. Mchoro wa Monalisa hautoi tafsiri wala maana yoyote, hivyo mchoro huo kubaki kuwa fumbo.

2. Mchoro wa Monalisa hauna maelezo wala maandishi yoyote yanayoweze kuonesha maana na nini hasa malengo ya mchoro huo, hivyo kubaki kuwa fumbo.

402px-Mona_Lisa%2C_by_Leonardo_da_Vinci%2C_from_C2RMF_retouched.jpg
 
Back
Top Bottom