Naomba kufahamu haya kuhusu Malcom X, Elijah Mohamed na Minister Farrakhan

Naomba kufahamu haya kuhusu Malcom X, Elijah Mohamed na Minister Farrakhan

Kakumamoto

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2015
Posts
1,237
Reaction score
1,696
Habari Wanajamvi,

kuna taarifa/story ambayo mimi sijaipata vizuri na napenda wanye uelewa watuhadithie.

Ni kwamba Malcom X alifundishwa Uislam na Elijah Mohamed lakini inaonekana Malcom alizisha uanaharakati na kufahamika zaidi kitu ambacho hakikumfurahisha Elijah, na pia Farrakhan hakuwa akimfurahia Malcom japo walikuwa ni marafiki.

Na hata kifo cha Malcom inasemekana Elijah na Farrakhan wanahusika. Na pia kuna ishu ya mtoto wa kike wa Malcom pia inahusishwa?! Nani anakisa hiki atufahamishe zaidi?
 

Attachments

  • FB_IMG_1682721521551.jpg
    FB_IMG_1682721521551.jpg
    31.7 KB · Views: 15
  • FB_IMG_1682721415126.jpg
    FB_IMG_1682721415126.jpg
    22.3 KB · Views: 13
Kwa kifupi Malcom X kauliwa na CIA, baada ya kuwa maarufu alikuwa na ego, pia kulikuwa na kawivu flani kutoka kwa Elijah Muhamad sababu jamaa alikuwa kaanza kukubalika sana na alimwona alichokuwa anafanya anazidisha sana alimwambia apunguze jamaa hakutaka kumsikiliza. Tafuta documentary who killed Malcom X kwa habari zaidi
 
Nani kamuua Malcolm? I have never asked myself this question. Walibishana na Elijah Muhammad kuhusu maoni aliyosema Malcolm baada ya Kennedy kuuawa,"It is a case of roosters coming home to roost";kwamba kama Kennedy kauawa,huo ni uovu wanaotutendea Wazungu kila siku,umewarudia wao.
Ndio Elijah Muhammad akasema,"Wewe,,kaa kimya. Kama Kennedy kauawa,we(Black Muslims) don't have to make any comments." Elijah Muhammad was right. Ile March to Washington ya Negroes iliyoongozwa na Martin Luther King Jr,ilifanyika wakati Kennedy alipokuwa rais.
Lakini kifo cha Malcolm,kama kifo cha Martin Luther Kingjr,most probably kilikuwa kazi ya American government.
I cite these various revolutions, brothers and sisters, to show you, you don’t have a peaceful revolution. You don’t have a turn-the-other-cheek revolution. There is no such thing as a nonviolent revolution. The only kind of revolution that’s nonviolent is the Negro revolution, the only revolution based on loving your enemy is the Negro revolution. The only revolution in which the goal is a desegregated lunch counter, a desegregated theater, a desegregated park, and a desegregated public toilet; you can sit down next to white folks on the toilet
 
Tofauti kubwa kati ya Elijah Mohamed na Malcom Hadi Malcom anaondoka NOI ilitokana na Malcom kuelewa Uislamu halisi tofauti na alivyokuwa akifundisha Elijah,Malcom aliweza pia juju uhuni wa Elijah kuhusu wanawake na pesa akaanza kumkosoa Elijah.Vurugu na hata kifo Cha Malcom vilitokana na ukweli huu.
 
Tofauti kubwa kati ya Elijah Mohamed na Malcom Hadi Malcom anaondoka NOI ilitokana na Malcom kuelewa Uislamu halisi tofauti na alivyokuwa akifundisha Elijah,Malcom aliweza pia juju uhuni wa Elijah kuhusu wanawake na pesa akaanza kumkosoa Elijah.Vurugu na hata kifo Cha Malcom vilitokana na ukweli huu.
Hii iko deep sana, nadhani kuna kitu kinafichwa sababu Elijah alikuwa akiheahimika sana sana, lakini kuna mambo ya Elijah hayakuwa sawa.
 
Cheki movie ya godfather of harlem,yamegusia mengi kuhusiana na maisha,harakati hadi kifo cha malcom x
 
Nitakuja na uzi maalaumu wenye uchambuzi wa ndani kabisa kuhusu NOI ,Malcom X na harakati zake zote za kimaisha .

Utakuwa evidence based katika kipa kipengele nishakusanya audio clips video now namalizia Kitabu cha tatu kabla ya kupanga mtiririko vizuri.
 
Nitakuja na uzi maalaumu wenye uchambuzi wa ndani kabisa kuhusu NOI ,Malcom X na harakati zake zote za kimaisha .

Utakuwa evidence based katika kipa kipengele nishakusanya audio clips video now namalizia Kitabu cha tatu kabla ya kupanga mtiririko vizuri.

Jambo jema,ila naomba iwe balanced achana na illusions kama za mzee said.
 
Jambo jema,ila naomba iwe balanced achana na illusions kama za mzee said.
Evidence based hakutokuwa na hayo mambo ,source zaidi ya moja na wahusika wakihojiwa hapo inakuwa rahisi kwenda na ukweli asilimia 90%.
 
Ninatafsiri Outobiography ya Malcom X. Baada ya mwezi itakuwa tayari. Walijiita taifa la kiislamu. Farakhan aliwahi kusikika akisema kuwa msaliti wa taifa huuwawa, na ndivyo walivyofanya, waliuua msaliti. Hata mtoto wa Malcom X mmoja mapepe mapepe alishtakiwa kwa kula njama za kutaka kumuua Farakhan kulipiza mauaji ya baba yake. Na wauaji watatu walioshikwa kwa mauaji ya MalcomX walikuwa memba wa National Islam. Lakini mtoto mwingine wa Malcom akataka kuwashtaki CIA kwa mauaji ya baba yake.

Utata hauwezi kufumbuliwa maana CIA ni wajanja wa kuweza kufanya Nation Islam ndiyo wahusika huku NOI nao wakiwa na sababu za msingi kutaka kumuua Malcom.
 
A Farrakhan aura pause on the pork,

You eat from the bowl while your dog needs a fork,
 
Malcolm X au Malik Al Shabazz hakupendezwa na NOI na hasa kiongozi wake Elijah Muhaammad kwa kufuata mafundisho tofauti ya Uislam. Walitofautiana kiitikadi za kisiasa kwa sababu Uislam hauna ubaguzi baina ya rangi wakati Elijah alichochea chuki ya weusi dhidi ya weupe kama kulipa kisasi kwa ubaguzi wao. Katika kitabu cha ALI, A Life, mwandishi anaeleza jinsi hata Muhammad Ali alivyokuwa akipata tabu kwa kuwa aliwaamini wote kama kiongozi wa Uislam Marekani. Inasemekana chuki ya Elijah kwa Malcolm X ni kwa sababu alipata wafuasi wengi na alikuwa akitekeleza dini hasa wakati Elijah alionekana ni mhuni hasa kwa kupenda pesa na wanawake
 
Back
Top Bottom