Naomba kufahamu hospital ya macho inayotibu vizuri kwa gharama nafuu ukiachana na CCBRT

Naomba kufahamu hospital ya macho inayotibu vizuri kwa gharama nafuu ukiachana na CCBRT

fatherhood

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
537
Reaction score
556
Habari JF

Sambamba na kichwa cha habari hapo juu naomba kufahamishwa hospitali ya macho nzuri inayotibu kwa bei nafuu ukiachana na CCBRT ya Msasani Masaki.

Note . Kwa hapa Dar es Salaam
 
Honestly, najua CCBRT tu ndiyo kwa uhakika...
 
Nilitibiwa ccbrt 2017 mpk Leo nipo fresh we jichange ukapate tiba mkuu au unataka hospital za vichochoroni
 
Nenda Dr. Agarwal Morocco hapo, pale hata CCBRT hawafui dafu. Yanii teknolojia ya hali ya juu sana.
Kuna ndugu yangu alienda CCBRT ila kuna vipimo hakufanyiwa, ila hapo Agarwal aise aliwekwa mitambo na akaelewa shida ilikua nini
Ko nikifika Morocco naulizaje

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kupimwa macho, KCMC-Moshi nikambiwa glass za macho zimekufa, nikajaribu lens zote zilikataa. Nikaambiwa tiba ni operation (sijui ndo kuchunwa). Sikuwahi kurudi kwa sababu;
1. Uchumi.
2. Uoga.
Tatizo kubwa hasa ni Poor Distance Vision. Ninafikiria kurudi.

USHAURI WOWOTE, Kama kubadili hospitali.

Ahsante.
 
Nenda Dr. Agarwal Morocco hapo, pale hata CCBRT hawafui dafu. Yanii teknolojia ya hali ya juu sana.
Kuna ndugu yangu alienda CCBRT ila kuna vipimo hakufanyiwa, ila hapo Agarwal aise aliwekwa mitambo na akaelewa shida ilikua nini
Kaka hapo Dr Agarwal wapo vizuri ndiyo sikatai ila mwambie jamaa ajichange bei yao sio ya kitoto yei zao zipo juu kichizi yani
 
Kaka hapo Dr Agarwal wapo vizuri ndiyo sikatai ila mwambie jamaa ajichange bei yao sio ya kitoto yei zao zipo juu kichizi yani
Hawa jama walinirudisha barabarani kwa kunichoma kale ka sindano kadogo kama mwiba machoni na macho yangu yakapona kabisa, kwani gharama nini?
 
Je mtu anayepoteza kuona au kuona hafifu kwa sabab ya uzee nae anatibika?
Je humu mnaisema bei kubwa bila kutaja wastan mnatusaidiaje.
How expensive is expensive!
 
Back
Top Bottom