hmaloh
Senior Member
- Nov 22, 2018
- 162
- 314
Habarini ndugu zangu wapendwa wanajamvi,
Naomba kufahamu ikiwa inawezekana kama mzazi kuwajibishwa kwa kosa alilofanya mtoto wangu. Hali iko hivi: hapa mtaani kuna mzee fulani anasema anataka kunipeleka kwenye vyombo vya sheria kwa sababu binti yangu alivunja kioo cha gari yake.
Walikuwa watoto wengi wakicheza mchezo wa kurushiana mawe, ila bahati mbaya kioo kilivunjwa na binti yangu.
Mzee huyo aliniita kwa ajili ya uharibifu uliofanyika, nami nilifika na kumwambia nitamlipa pesa hiyo ya kioo, ila sasa hivi sipo vizuri kifedha. Cha ajabu ni kwamba, mzee huyo anaendelea kunitishia na kuniambia atanionesha kwa sababu sijamlipa pesa hiyo.
Je, sheria inasemaje kuhusu suala hili? Naweza kuchukuliwa hatua kwa kosa lililofanywa na mwanangu?
NB: Kwa taarifa, binti yangu ana umri wa miaka 6.