Habari ndugu zangu,Naomba kujuzwa kwa mwenye kufahamu kuhusu haya magonjwa yasiyoambukizwa namna yanavyoenea kwa kasi,Miaka ya nyuma chakula chetu kikuu kilikuwa Wali na Ugali lakini kasi ya magonjwa haya haikuwa kubwa kama ilivyo leo, Lakini leo hii tunaambiwa moja ya sababu ya magonjwa kama presha ni kula ugali na Wali kwa wingi, Sasa naomba kujua tunatakiwa kula nini ili kuepuka madhara ya magonjwa haya? Asubui tule nini, Mchana tule nini, Na usiku tule nini? Karibuni.