Naomba kufahamu kuhusu Power Mabula

Naomba kufahamu kuhusu Power Mabula

Kai ni Body builder kama umemjua natumai unawajua pia Strong Man kama huwajui wafuatilie.

Strong man wana Size kubwa ya mwili kuliko Body builder na sifa ya kuwa Strong man uwe na mwili miraba 7 wakuzaliwa....Mabula mwili mkubwa kuzaliwa Kai ana mwili mdogo kuzaliwa kuijaza sana through ujazo wake unaenda na Dimension ya Anatomy ya mifupa yake.
Wewe unamuelezea Kai Green wakati donlucchese anamuelezea Great Khali mwanamieleka.
 
Alikuwa na show yake moja, anawekewa jiwe kubwa sana kifuani, (sio Meko). Uzito tu wa like jiwe unakufanya upate korona na ukiwa umeacha kiasi kikubwa sana cha mboji sakafuni.
Akishawekewa jiwe hilo, hutafutwa mtu mwenye nguvu zake, Kisha huanza kulipiga na nyundo kubwa Sana.
Power Mabula alistaafu michezo yake baada ya kwenda Rukwa, sumbawanga, huko alipita mitaani akiwa juu ya Land Rover 109, akionyesha promo.
Kuna mtaa unaitwa Mazwi, akakuta mtoto wa miaka mitano analisukuma Scania na trela lake, akastaabu sana, akauliza baba yako Yuko wapi? Akajibiwa kaenda kuuleta mlima uleeeee, auweke jirani na nyumba yetu

Kwahiyo yeye na michezo yake yote akajiona cha mtoto???🤣🤣
 
Great Kai na huyo jamaa hapo Jamaa ni mkubwa ki Size ya mwili, Kai ana misuli tu.
Yaani Great Khali who is over 7 ft unataka mfananisha na huyu mtu ambaye roughly ni kama ana 6.6ft hivi...

Ila kama ni yule bodybuilder Kai Greene, yule mwamba ni mfupi size ya kawaida tu 1.7 meter hivi
 
ingekuwa ni miaka hii angekuwa zake ughaibuni akishindana na watu wenye nguvu kama yeye kwenye mashindano ya deadlift. this competition is for people like power mabula, very professional and well organized.
https://youtu.be/rVRvAsJKf6Y
 
Wanefili ndio kinanani
Watu wanaosemekana waliishi zamani, yaani watu wa zamani ndio walikuwa na miili hiyo sisi tumetokana tu na mabadiliko

Kwahiyo kwa ufahamu wangu nahisi kina Mabula ni mabaki ya mwisho mwisho ya watu wa zamani, tazama yale mapiramidi ya misri zile nguzo na matofali yake, hakukuwa na greda lakini inasemekana watu waliyabeba kujengea, rejea stori za Ng'wana Malundi inasemekana alikua na unyayo mkubwa mno hivyo lazima hata mwili wake ulikuwa mkubwa

Ndio ilikuwa miili ya zamani
 
Power Mabula kitambo sana,kweli kila zama na kitabu chake,
Alikua anaweka ubao kifuani kisha zinapita Pikipiki juu ya kifua chake,alikua akizuwia pikipiki kwa meno! Pikipiki inafungwa kamba kisha ile kamba yeye anaiuma na meno,alikua akizuwia gari mbili kwa wakati mmoja,gari inafunga kamba kisha ila kamba anaishika kwa mkono wa kushoto na gari ya pili kwa mkono wa kulia,gari zinapiga resi ila zipo pale pale!

Sijui hali hii aliiweza kutokana na mazoezi au alikua tu na nguvu za kuzaliwa nazo,inaweza kua ni Inborn talent.
Pamoja na mwili wa asili nafikiri alikuwa na mzingaombwe pia
 
Yaani Great Khali who is over 7 ft unataka mfananisha na huyu mtu ambaye roughly ni kama ana 6.6ft hivi...

Ila kama ni yule bodybuilder Kai Greene, yule mwamba ni mfupi size ya kawaida tu 1.7 meter hivi
Nani amepata kumuona Great Khali kwa macho? Na Mabula kwa macho?

Vipimo vya Great Khali tunaweza kuvipata hata Google, vya Mabula je? Tunajuaje kama Khali anamzidi Mabula?
 
Power Mabula alishafariki na kuzikwa Morogoro nadhani ilikuwa 2015 kama sijakosea
 
Mkuu nampenyezea MAMA kimemo.... hatakuacha hv hv
Alikuwa na show yake moja, anawekewa jiwe kubwa sana kifuani, (sio Meko). Uzito tu wa like jiwe unakufanya upate korona na ukiwa umeacha kiasi kikubwa sana cha mboji sakafuni.
Akishawekewa jiwe hilo, hutafutwa mtu mwenye nguvu zake, Kisha huanza kulipiga na nyundo kubwa Sana.
Power Mabula alistaafu michezo yake baada ya kwenda Rukwa, sumbawanga, huko alipita mitaani akiwa juu ya Land Rover 109, akionyesha promo.
Kuna mtaa unaitwa Mazwi, akakuta mtoto wa miaka mitano analisukuma Scania na trela lake, akastaabu sana, akauliza baba yako Yuko wapi? Akajibiwa kaenda kuuleta mlima uleeeee, auweke jirani na nyumba yetu

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom