Alikuwa na show yake moja, anawekewa jiwe kubwa sana kifuani, (sio Meko). Uzito tu wa like jiwe unakufanya upate korona na ukiwa umeacha kiasi kikubwa sana cha mboji sakafuni.
Akishawekewa jiwe hilo, hutafutwa mtu mwenye nguvu zake, Kisha huanza kulipiga na nyundo kubwa Sana.
Power Mabula alistaafu michezo yake baada ya kwenda Rukwa,
sumbawanga, huko alipita mitaani akiwa juu ya Land Rover 109, akionyesha promo.
Kuna mtaa unaitwa Mazwi, akakuta mtoto wa miaka mitano analisukuma Scania na trela lake, akastaabu sana, akauliza baba yako Yuko wapi? Akajibiwa kaenda kuuleta mlima uleeeee, auweke jirani na nyumba yetu