Naomba kufahamu maana ya haya maneno yanayotumika sana uswazi

Naomba kufahamu maana ya haya maneno yanayotumika sana uswazi

Ngoja waje kukupa miongozo...

Sio kivile - sio sawa, sio vizuri... Kivuruge - fujo, ghasia,vurugu... Bandidu - Muhalifu, wizi, mauaji... Ushubwada - uzushi, upotoshaji, kudanganya... Mgaigai - ukorofi, tabia mbaya.. Macho kuona - kuamini, kutambua, kushuhudia... Kausha damu - kukasirika, kuchukia... Harakati - shughuli... Udwanzi - ujanja, ustadi...
 
kuna baadhi ya maneno yananikumbusha mbali nikisia mfano bandidu hili linanikumbusha wimbo wa mtoto Iddi wa juma nature katika verse yake moja aliimba hivii Iddi ni mtoto mwenye sura ya KIBANDIDU iddi ni mtoto wa kwanza wa mzee hamidu

Sio kivile hii inanikumbusha katika nyimbo ya daimond inaitwa nalia na mengi ambapo diamond anaimba hivii mi mkwanja nikamwaga mamaa japo SIO KIVILE ila kwangu ya maana

Kivuruge hii inanikumbusha wimbo wa nandy unaitwa kivuruge

macho kuona hii inanikumbusha wimbo wa daz baba unaitwa namba nane ambapo daz baba anaimba MACHO KUONA wakimuona hawatasita kumfata

harakati hii inanikumbusha wimbo wa bye bye wa joh makin ambapo anaimba HARAKATI ni magirini nipo kwenye nchi ya mungu hawafati mbele wamemuweka kaisari mtaaani moto jela kuna wapindisha hawanyooki
 
Tashtiti ni vuruguuu. Kuhangaika.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom