Naomba kufahamu Madhara ya kupeana talaka baada ya ndoa Kuvunjika

Naomba kufahamu Madhara ya kupeana talaka baada ya ndoa Kuvunjika

Wanaume wengi wanaathirika kisaikolojia kutokana na mali kupigwa mgao, ila wewe kama hiyo haitakuathiri kivyovyote basi ni ngumu kuwepo kwa athari nyingine.
 
Mimi ni mkristo na nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 8 na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili sasa ila kuna jambo nililikosea kwa mkewangu na sasa nataka nimwambie ukweli kuhusu hilo sasa kutokana na uzoefu kumhusu kwa kaliba yake naona kabisa ataenda kukiwasha isivyo kawaida na kwa asilimia 89.6% anaweza kudai talaka (namuwazia tu kichwani🙁) sasa kabla sijakubali atakachokidai naomba kufahamu kwa wale ambao mmeshapitia hii situation ya ndoa kuvunjika mpaka kupeana talaka..

Je kuna madhara yoyote yanaweza kutokea kama mmekaa kwenye ndoa kwa muda mrefu kiasi hiki ukiachana na kugawana mali sijui nini ... Je haya mambo ya kupeana ttalaka inaweza kuniletea shida ya kisaikolojia au kiroho nikakengeuka.. ? mliopita kwenye hii situation naomba uzoefu wenu, nitashukuru sana kabla sijaaamua ..🙏
Nina haya ya kusema juu ya hili, ingawa sijapitia hali hiyo, ila nina ndugu yangu ameshapitia hilo tena kwa kupeana talaka mahakamani.

Madhara ni haya;

1. Watoto wataenda kulelewa na mzazi mwingine (Yaani wewe ukioa, huyo mama si mama yao mzazi, au yeye akiolewa, huyo baba siyo baba yao mzazi). Changamoto hapa ipo kwenye namna watakavyolelelwa. Baba au mama wa kambo, ni wachache sana wenye roho nzuri kwa watoto wa wenza wao. Ukiwepo mwenye mtoto, mtoto ataonyeshwa mapenzi ya kuzuga, ukitoka tu, jehanamu inamuwakia

2. Siku hizi, mali inagawanywa kwa watalaka pasu kwa pasu. Hakuna cha kusema hii ni ya watoto, labda kama mmoja aamue kuacha iwe hivyo. Ila mkienda mahakamani, ni kwamba pasu itahusika. Hao watoto hata kama mngekuwa hamna mali ya kugawana, bado wangelelewa na atakayebaki nao kwa ushirika.

3. Huko kwenye ndoa mpya, kila mzazi mwenzio anapotaka kuwaona watoto, kunaweza kukawa na vurugu. Yaani, kama watoto watabaki kwa mama yao ambaye ameolewa na mwanaume mwingine, kila ukionekana kwake, lazima mume mpya apatwe na mashaka. Maana kupasha kiporo wala hakuhitaji moto mwingi. Na hii hata kwako, kama watoto utabaki nao, mama yao akija kuwaona, lazima mke mpya atapata wasiwasi au wivu. Sababu ni ile ile, ya kiporo kukipasha hakihitajo motot mwingi.

4. Huko kwenye ndoa mpya, kila mmoja hataweza kufunga ndoa tena, ila ataishi na mwenza mpya bila ndoa. Maana ndoa za kikristo (hasa wakatoliki), kufunga ndoa nyingine kanisani, ni hadi kifo kiwatenganishe. Yaani mmoja akifa, aliyebaki anaweza akafunga ndoa tena kanisani.

5. Watoto kukosa malezi ya upande mmoja.

CC mamdogo Amehlo
 
Kama hauwezi kustahimili ndoa, mwambie tu ili muachane... Yaani hadi una umri wa miaka minane katika ndoa haujui mkiachana utapata hasara zipi! Kweli....

Mkiachana wala hakuna madhara mkuu... Utaishi peke yako kama mfalme na utaheshimika sana kwa sababu wewe ni mwamba umeachana na mkeo.
Katika nyakati tofauti kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako itanidhuru then kuna nyakati kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako utakuwa poa tuu sasa nipo njia panda nielekee upande upi kuhusu mali sina shida na hilo ntamwachia tu maana ni za watoto
 
Mimi ni mkristo na nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 8 na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili sasa ila kuna jambo nililikosea kwa mkewangu na sasa nataka nimwambie ukweli kuhusu hilo sasa kutokana na uzoefu kumhusu kwa kaliba yake naona kabisa ataenda kukiwasha isivyo kawaida na kwa asilimia 89.6% anaweza kudai talaka (namuwazia tu kichwani🙁).

Sasa kabla sijakubali atakachokidai naomba kufahamu kwa wale ambao mmeshapitia hii situation ya ndoa kuvunjika mpaka kupeana talaka.

Je, kuna madhara yoyote yanaweza kutokea kama mmekaa kwenye ndoa kwa muda mrefu kiasi hiki ukiachana na kugawana mali sijui nini?

Je, haya mambo ya kupeana talaka inaweza kuniletea shida ya kisaikolojia au kiroho nikakengeuka?

Mliopita kwenye hii situation naomba uzoefu wenu, nitashukuru sana kabla sijaaamua ..🙏

Yaani umekaa na mke wako wako kwenye ndoa kwa miaka 8! Mkabarikiwa na watoto 2! Bila shaka mtakuwa mnaishi kwenu!!

Halafu unakuja na porojo za aina gani tena!! Mbaya zaidi kwenye ndoa za Kikristo, ni kifo tu ndicho kinacho watenganisha!!

Aisee kama una mtoto wa nje ya ndoa, ni bora ukamtoa tu sadaka. Wajulishe wazazi wako/ndugu zako baadhi ili wamtambue kimya kimya. Ila usijaribu kuivunja ndoa yako kwa vitu vya kijinga.

Huyo mke uliye naye, leo hii unaweza ukamuona ni wa kawaida! Kwa sababu tu umemzoea. Ila siku asipokuwepo kabisa kwenye maisha yako, utataabika sana.

Nakushauri umpende na kumheshimu daima. Hapa duniani kuna wanawake wengi wazuri! Ila wife material, ni wachache sana.
 
katika nyakati tofauti kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako itanidhuru then kuna nyakati kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako utakuwa poa tuu sasa nipo njia panda nielekee upande upi kuhusu mali sina shida na hilo ntamwachia tu maana ni za watoto
Jaribu kumuacha, halafu uone madhara yake. Yaani from nowhere tu umuache mtu ambaye hajakukosea kitu chochote! Aisee masononeko yake yatakutesa kwenye maisha yako yote.
 
Maamuzi ya kipumbavu na ubinafsi hapa ushaleta viumbe dunia(watoto) unaenda kuwaandalia mateso makubwa kwa tamaa zako za kishamba .

Mtu mzima unafanya mambo ya hovyo hata mkiachana ukaoa ni yale yale dunia haina jipya.

Hapa ndo utaona ubinafsi wa binadamu haswa wazazi kila mtu anajua kwamba ataoa au ataolewa kwingine meanwhile watoto watapata mateso ya kudumu kwa maamuzi yenu ya kishamba..

Ndoa ina miaka 8 ni mingi kwa wastani na mnaweza kusameana ..90% waliovunja ndoa zao ni majuto tu wanakutana na wale wale hamna kipya .

Umekosea jishushe na kiri kosa usifikirie kuvunja ndoa ni kuwakatili watoto wako.
 
Wanaume wengi wanaathirika kisaikolojia kutokana na mali kupigwa mgao, ila wewe kama hiyo haitakuathiri kivyovyote basi ni ngumu kuwepo kwa athari nyingine.
Asante mkuu kuhusu mali sina shida nazo hata akibaki nazo wasiwasi wangu ulikuwa naweza kupata madhara mengine ya kisaikolojia au ya kiroho nikashindwa kutimiza ndoto zangu..
 
Maamuzi ya kipumbavu na ubinafsi hapa ushaleta viumbe dunia(watoto) unaenda kuwaandalia mateso makubwa kwa tamaa zako za kishamba .


Mtu mzima unafanya mambo ya hovyo hata mkiachana ukaoa ni yale yale dunia haina jipya.


Hapa ndo utaona ubinafsi wa binadamu haswa wazazi kila mtu anajua kwamba ataoa au ataolewa kwingine meanwhile watoto watapata mateso ya kudumu kwa maamuzi yenu ya kishamba..

Ndoa ina miaka 8 ni mingi kwa wastani na mnaweza kusameana ..90% waliovunja ndoa zao ni majuto tu wanakutana na wale wale hamna kipya .

Umekosea jishushe na kiri kosa usifikirie kuvunja ndoa ni kuwakatili watoto wako.
Asante mkuu kwa husia nzuri ila umenizodoa but nashukuru.. thanks in advance
 
asante mkuu kuhusu mali sina shida nazo hata akibaki nazo wasiwasi wangu ulikuwa naweza kupata madhara mengine ya kisaikolojia au ya kiroho nikashindwa kutimiza ndoto zangu..
Lakini pia kama bado unampenda mkeo, ni bora hilo swala ukalifikiria in deep zaidi mkuu.
 
katika nyakati tofauti kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako itanidhuru then kuna nyakati kuna sauti inaniambia ukiachana na mkewako utakuwa poa tuu sasa nipo njia panda nielekee upande upi kuhusu mali sina shida na hilo ntamwachia tu maana ni za watoto
Mcanada
Kama kuna ishu inaweza haribu ndoa yako, nakushauri usimwambie mkeo. Tunza siri, sisi sote humu tuna siri zetu ila tumemeza pini.... Tupo kimyaaaa maisha yanasonga.

Sisi wanaume tuna siri nyingi sana, tunajua wenyewe na hatuvunji ndoa. Hata zikifahamika huko mbele tutakuwa tumeishafaulu kuzilea familia zetu kiasi kwamba madhara hayatakuwa makubwa kama tungezisema mapema.

Mimi huwa nawaza tu, nilivyo mkorofi na jinsi huyu mke wangu anavyonivumilia. Halafu leo niachane naye, then itokee nitafute mwingine nianze kumfundisha nilivyo hadi anielewe, naona huo muda sina tena mkuu.

Piga kimyaaaaa. Maisha yaendelee, ndoa ni tunu katika jamii za kiafrika. Usiivunje kwa kitu unachoweza kukizuia. Tunza siri.
 
Back
Top Bottom