Naomba kufahamu makadirio ya bati na mbao kuezeka nyumba hii

Mkuu nina kautaalamu kidogo cha kuezeka ila kwa calculation yako hii umeenda mbali mno!

Ila nimekukubali sana , i wish ungenipiga msasa kidogo.
Mkuu mchoro wenyewe huu hapa
 

Attachments

  • Screenshot_20221224-161537.png
    70.5 KB · Views: 193
 

Hii ramani yako mchoraji hakutumia scale, mana upande ambao ni mrefu (10.9m) unaonekana ni mfupi kuliko upande ambao ni mfupi (8.5m). Scale ni muhimu sana ktk uchoraji vinginevyo ramani itakuja ikusumbue kwenye vipimo mfano ukiangalia hicho chumba chenye mita 4.5, ukafanya hesabu utagundua hicho kikabati kina 80cm lakini ukiangalia mchoro unaona ukuta unaotenganisha hizo kabati (closet) upo katikati ya korido ambayo ina 1.2m hivyo pattern inaonesha closet ina 60cm lakini vipimo vinaonesha closet ina 80cm, kama angetumia scale huo ukuta usingekaa katikati kama unavyoonekana. Yote kwa yote ukiondoa hizo varanda, mfumo uliobaki kutokana na ramani yako ni wa mfumo wa mapaa manne (kunakuwa hakuna ukuta wa gable baada ya stop course)
 
Nini madhara yake mkuu?
 
Na je makadirio ya bati na mbao kuna mabadiliko?
Mabadiliko yatakuwepo japo sio kwa kiasi kikubwa, mfumo wa mapaa manne unakuwa na wastage nyingi ya material, sio kwa bati tu hata kwa upande wa mbao. Faida yake ni kwamba utakuwa unavuna maji mengi kipindi cha mvua. Mfumo wa mapaa manne unapendeza zaidi kama nyumba yako ina umbo la mstatili mfano 5m kwa 9m, lakini kama nyumba ina umbo la mraba au vipimo vyake vimekaribiana sana mfano 5m kwa 5.5m paa litatokea kama mwamvuli
 
Mabadiliko ya ongezeko au kupungua?
 
 
 
Ramani yako ina makosa kadhaa, dirisha la choo cha public limeangalia choo cha chumba cha master..lakini pia kiusalama mlango wa jikoni unatakiwa ufungukie nje ili iwe rahisi kujiokoa inapotekea hatari kama moto n.k, kama bado hujapachika frem za milango badilisha uelekeo wa frem

Tukija kwenye upauaji, kama utapaua mapaa manne kingpost za katikati zitakaribiana sana kutokana na umbo la ramani yako (mraba), na pengine inaweza ikawa na kingpost moja tu mana wakati mwingine kingpost zikikaribiana sana, kingpost nyingine huwa inauliwa ili kusave mbao japo muonekano wake unakuwa haupendezi
 
Ni kweli mkuu dirisha la choo cha public linafungukia choo cha master. Hilo nimekubali iwe hivyo. Fremu bado sijaweka.
 
Ni kweli mkuu dirisha la choo cha public linafungukia choo cha master. Hilo nimekubali iwe hivyo. Fremu bado sijaweka.
Choo cha public hakitakuwa na chemba, sijui lakini hawa watu wa bomba watatumia maarifa gani hapo
 
Mkuu Mimi nataka kujenga nyumba 13.2m x 9.5m naomba unikadirie bati
Hii nyumba kwa mbele itainekana hivi au kama vipi ntaweka hanamu mbili hapo mbele.
 

Attachments

  • IMG_20230703_195245~2.jpg
    27.5 KB · Views: 135

Uzi mzuri sana, we jamaa uko deep sana kwenye hii kitu.
 
Natumae mleta mada ulipata muongozo...
 
Mkuu Mimi nataka kujenga nyumba 13.2m x 9.5m naomba unikadirie bati
Hii nyumba kwa mbele itainekana hivi au kama vipi ntaweka hanamu mbili hapo mbele.
Itabidi tuwasiliane ndg maana hapa nilikuwa natoa elimu ili kila mmoja aweze kufanya makadirio mwenyewe, in case kama mtu atataka nimfanyie makadirio hiyo tena itakuwa ni biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…