Naomba kufahamu msimu wa bei nzuri ya Vitunguu Maji

SIR.NOM

Member
Joined
Sep 8, 2012
Posts
78
Reaction score
24
Wadau habarini,

Naombaen ushaur kwa wazoefu wa kilimo cha VITUNGUU MAJI.Nimeshaanza mradi wa kulima hili zao,ndoto yangu ni kulima Ekari 3.

Ila hofu yangu ni uhakika wa SOKO,kwa muda ntakaokuja kuvuna.Maana apa nategemea kuja kuvuna mwez wa 9 mwishoni hadi wa 10 hiv.

Ombi langu,naomba kujua uhakika wa bei nzuri sokoni kwa miezi hiyo kuanzia mwezi wa 9 hadi wa 11
 
Mkuu hongera sana upo mkoa gani yaani unapofanyia huo mradi ?
 
Ukisha vuna ondoa layer ya kwanza ya vitunguu, ondoa mizizi na ukake inch 5-7 kutoka kwenye shina au majani. Jenga kichanja, tandika gunia au mkeka. Anika vitunguu kwa wiki mbili.

Vikikauka ondoa teana ngozi ya juu ibaki ile kama karatasi. Hifadhi vitunguu kwenye mifuko ya wavu. Weka ghalani, hakikisha ghala lina hewa ya kutosha.

Kwa hali hii unaweza kuvihifadhi hata kwa miezi sita.

 
Hii nimeipenda!
 
Huku niliko kilo moja tunauziwa 2500 vipi tunapigwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…