Naomba kufahamu tofauti kati ya ushuru na kodi

Naomba kufahamu tofauti kati ya ushuru na kodi

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
13,654
Reaction score
8,564
Nikiwa zangu nimepumzika muda huu na uchovu wa pilikapilika za hapa na pale ili nipate tonge kusogeza siku,basi nimewasha tv nakutana na mtangazaji ana wahoji wafanyabiashara nini maana ya kodi na ushuru ni nini mpaka muda huu jibu halijapatikana nimeona nileta hapa jamvini ili nami nipate kuelewa kodi ni nini na ushuru ni nini?
 
WANAJAMVI, Leo nikiwa kwenye basi nikitoka Dar kuelekea Mwanza, kulitokea mabishano kwa JIRANI zangu kwenye siti ndani ya Basi, wakibishania maana au tofauti ya neno kodi, ushuru, forodha. Sasa kwa kuwa mimi siyafahamu nilikaa kimya nasikilizia huku wakifurahi. Nimeamua niombe majibu na Elimu humu jf.
Tafadhali sana karibuni tuelimishane.
 
Kodi huwa inalipwa ndani ya muda maalumu mfano mwezi au mwaka ambayo hulipwa kwa kukokotoa asilimia Fulani ya faida inayotarajiwa kupatikana ndani ya kipindi au muda niliotaja hapo juu lakini ushuru in malipo ya kila Sikh ambayo mfanyabiashara anatozwa kugharamia Huduma mfano kila gari ikiingia stand hutuzwa sh 500 kama ushuru, au mnadani, kila anaeingia kuuza kitu chochote lazima atoe ushuru kwa ajili ya usafi.
 
Kodi(tax)=compulsory contribution levied by the gvt for a particular good or service inaweza kuwa VAT on Income tax, na hii ipo chini ya serikali kuu hapa Tz na inatambulika na kulindwa na katiba refer Income tax act 2000 if am not mistaken a yr, but
Ushuru(tariff) hii ni michango au tozo ambazo hutolewa pia kwaajili ya huduma au bidhaa isipokuwa tu ipo chini ya sheria ndogondogo za mahali husika na hubadilika mara kwa mara kutokana na uhitaji chini ya mamlaka husika mfano local gvt act inawapa watendaji wa serikali za mtaa uwezo wa kupanga tozo juu ya kitu fulani au kuiondoa pia na baadhi ya taasisi za serikali tofauti pia iliyopo kati ya hii na kodi ni kwamba ili kodi ibadilike ina mlolongo mrefu ni lazima ipite hadi bungeni ibadilishwe kisheria tofauti na ushuru ikikaa tu bodi au kamati fulani wanafanya watakavyo.ni somo pana kidogo niishie hapo kwa leo
 
Kodi huwa inalipwa ndani ya muda maalumu mfano mwezi au mwaka ambayo hulipwa kwa kukokotoa asilimia Fulani ya faida inayotarajiwa kupatikana ndani ya kipindi au muda niliotaja hapo juu lakini ushuru in malipo ya kila Sikh ambayo mfanyabiashara anatozwa kugharamia Huduma mfano kila gari ikiingia stand hutuzwa sh 500 kama ushuru, au mnadani, kila anaeingia kuuza kitu chochote lazima atoe ushuru kwa ajili ya usafi.
Ahsante sana! ila forodha hujaigusia.
 
Nikiwa zangu nimepumzika muda huu na uchovu wa pilikapilika za hapa na pale ili nipate tonge kusogeza siku,basi nimewasha tv nakutana na mtangazaji ana wahoji wafanyabiashara nini maana ya kodi na ushuru ni nini mpaka muda huu jibu halijapatikana nimeona nileta hapa jamvini ili nami nipate kuelewa kodi ni nini na ushuru ni nini?
Niko SokoMatola wapi wewe?
 
Back
Top Bottom