Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unaweza kufanikiwa lakini usiwe tajiri, utajiri ni zaidi ya kufanikiwaHaya maneno mawili yananichanganya kidogo naomba mwenye uelewa aniandikie hapa nijifunze Kufanikiwa si ndio kutajirika huko au kutajirika ndio kufanikiwa kwenyewe mi sielewii.
Kufanikiwa ni kupata ulichotaka ulivyotaka.Haya maneno mawili yananichanganya kidogo naomba mwenye uelewa aniandikie hapa nijifunze Kufanikiwa si ndio kutajirika huko au kutajirika ndio kufanikiwa kwenyewe mi sielewii.
Kwa maelezo yako kufanikiwa ni zaidi ya kutajirika?Kufanikiwa ni kupata ulichotaka ulivyotaka.
Mfano, kuna profesa wangu mmoja alipanga kuwa Jaji, kufundisha Chuo Kikuu na kuandika kitabu. Alifanikiwa kufikisha lengo lake hilo.
Hapi amefanikiwa bila kujali kama alitajirika au hapana.
Kutajirika nako kupo kwa aina nyingi, lakini wengi wakiongelea kutajirika wanaongelea kiuchumi.
Kuna mtu ndoto yake ni kuwa baharia, akipata kazi ya ubaharia anakuwa kafanikiwa kwenye hilo, bila kujali atatajirika au hatatajirika.
Kuna mwingine anataka kuwa mbunge, lakininhafanikiwi katika hilo, anakuwa mfanyabiashara aliye tajiri sana kiuchumi, lakini hajafanikiwa kutumikia watu kama mbunge.
Kuna mwingine alitaka kuwa padri, lakini hakufanikiwa katika hilo, kaishia kuwa makamu wa rais.
Naam,Kwa maelezo yako kufanikiwa ni zaidi ya kutajirika?
mtu ni bilionea lakini alitaka ubunge akaukosa kwahiyo hajafanikiwa? Hapo umeenda kwenye mada nyingine
www.simplypsychology.org
Katika ngazi tano za Maslow za kufikia self-actualization, utajiri wa kiuchumi ni ngazi ya pili kutoka chini, maana yake ukimaliza utajiri kuna ngazi nyingine tatu za kupanda.Unaweza kuwa tajiri lakini huna mafanikio na unaweza kuwa umefanikiwa lakini huna utajiri.
www.simplypsychology.org