Kwa maelezo yako kufanikiwa ni zaidi ya kutajirika?
mtu ni bilionea lakini alitaka ubunge akaukosa kwahiyo hajafanikiwa? Hapo umeenda kwenye mada nyingine
Naam,
Nitakupa mfano.
Kuna tajiri bilionea mkubwa wa Kimarekani anaitwa Ted Turner. Yeye ndiye kaanzisha CNN, alikuja kuiuza baadaye. Katika watu wanaomiliki ardhi kubwa sana Marekani yeye pia yumo, kuna wakati alikuwa ndiye mtu binafsi wa kwanza anayemiliki ardhi sehemu kubwa zaidi Marekani.
Kuna siku alikuwa anafanyiwa mahojiano, akaulizwa, katika maisha yake anaona kuna mapungufu wapi? Wapi hajafanikiwa?
Akajibu kwamba, anaona hajafanikiwa katika maisha ya ndoa, alitamani sana awe na maisha ya ndoa yaliyonyooka bila talaka, lakini ndoa yake na Jane Fonda, muigiza sinema wa Kimarekani, iliishia kwenye talaka.
Kwa hivyo, yumkini mafanikio si kitu kimoja tu, yana nyanja mbalimbali, na katika upande wa biashara, uchumi, Ted Turner amefanikiwa sana, kafanya deals kubwa sana za mabilioni ya US dollar, anamiliki ardhi sehemu kubwa sana Marekani, lakini kwenye sehemu ya mafanikio ya maisha ya ndoa hata yeye mwenyewe anasema hajafanikiwa.
Na kama Ted Turner mwenyewe akiona kuwa maisha ya kudumu katika ndoa nyoofu ni kitu muhimu zaidi ya utajiri, kiujumla katika maisha yake atajiona hajafanikiwa, licha ya utajiri wa kiuchumi mkubwa sana alionao.
Kuna watu matajiri sana kiuchumi, lakini wanaona utajiri wao hauna purpose, na kwa sababu wanataka kuishi maisha ya purpose na kuacha legacy, licha ya utajiri wote huo wa kiuchumi, wanajiona hawajafanikiwa.
Kwa sababu, wanaona, utajiri unaweza kuupata hata kwa bahati nasibu, kitu chenye maana zaidi kwao na kuonekana kuwa ni mafanikio ni kuishi maisha ya purpose na kuacha legacy, mambo ya Abraham Maslow pyramid of needs hayo.
Watu wengi waliokuwa self actualized pesa si mafanikio, kuacha legacy ndiyo mafanikio.
Ndiyo maana unaweza kukuta mtu kama Julius Nyerere, amefariki hana pesa nyingi sana, lakini kuna watu wanaweza kusema kuwa kaumba nchi moja, kajenga nchi, kasaidia kukomboa nchi za Afrika, amefanya mambo makubwa ambayo mengine hata pesa haiwezi kuyafanya (of course ana mapungufu yake, lakini tuangakie achievements hapa).
Ukimlinganisha Nyerere ambaye amefariki bila hela nyingi na mtu kama Mobutu aliyefariki na mabilioni ya US dollar, watu wengi wanaweza kusema Nyerere amefanikiwa kuliko Mobutu kwa heshima aliyojijengea kimataifa, licha ya kushindwa kutimiza ndoto zake, lakini alikuwa na falsafa mpya, aliumba nchi moya, watu wake walimuheshimu na kumoenda sana, aliandika falsafa zake nyingi watu wanasoma na kumnukuu mpaka leo kama mtubwa jutoa muingozo, hivyo, hata bila ya kuwa na pesa nyingi, amefanikiwa kwa kiasi fulani.
Mobutu naye amefanikiwa katika wanaooenda ubadhirifu wa mali ya umma na utajiri uliokithiri.
Maslow's hierarchy of needs is a pyramid of the needs that motivate people. Individuals most basic needs, at the base of the pyramid, are physiological. Once they have fulfilled these needs, people move on to their safety needs, social well-being, self-esteem then ultimately their need for...