Ni ukweli uliowazi,
Tangu tronic ya bongo aichukue mchina, quality ya bidhaa zimekua chenga Kweli kweli, kabaki kutembelea jina na bidhaa chache ambazo naona bado hajazichakachua (extension,sockets na switches) .
Mwezi june tronic walifyatua bulb za led, wachuuzi tukazikimbilia mbio tukijua tutauzia jina, ila kuja kustuka ni chenga sana na zinafifia Kama mishumaa. Sahv sizioni Tena sokoni.
Sept katoa mainswitch ndogo za surface 2way-4wy na anaziuza Bei chini Kama hizi za kichina, kuanzia elfu 22, 25 na 27 kwa 2wy,3y na 4wy. ila ukikagua hazina ubora ule wa tronic tunaemjua (kazifunga fuse za uwezo mdg Sana)
Sahv pia anazo m/switch kubwa za kuchimbia za 4wy-6wy ila kazichakachua sana na kuzipachika fuse za mainswitch ndogo za surface anaziuza elfu 55, tofauti na zile orijino tulizozoea za elfu 67. Ukienda kichwa kichwa unapigwa.