Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

Maana yake JPM alianza shule ya msingi akiwa na miaka 8 (1967) na akasoma elimu hiyo kwa miaka 8 (mpaka 1974) au 9 (mpaka 1975), - sijui ilikuwaje mpaka kuwa na hiyo miaka 2 ya ziada.

Akaanza kidato cha kwanza akiwa na miaka 16 (1975) na kumaliza kidato cha 4 akiwa na miaka 19 (1978). Akajiunga Kidato cha 5 akiwa na miaka 20 (1979) na kumaliza akiwa na miaka 22 (1981) akapiga Diploma miaka 2 na kumaliza 1983 akiwa na miaka 24 na kwenda kufundisha Sengerema 1983 akiwa na miaka 23 labda ndio akamkuta Kangi yupo kidato cha 3 akiwa na miaka 20. Akamfundisha miaka 2 hiyo, 1983 na 1984.
 
Mkwawa ilikuwa ni A-Level/Chuo inayofundisha Sub Combination kama vile PM, CM, CB nk. Walikuwa wanasoma na somo lingine lililokuwa linaitwa Education, halafu wanafanya mtihani wa form six kisha wanaongeza mwaka mmoja wanasoma Education Methodology halafu wanatoka Na Diploma ya Ualimu,ukifaulu sana baada ya kumaliza JKT ilikuwa unaunganisha University. Kwa hiyo walikuwa wanasoma miaka MITATU Na siyo minne. Lengo lilikuwa kupata waalimu bora wa sekondari Na vyuo vya ualimu.
 
Mkwawa ilikuwa ni A-Level/Chuo inayofundisha Sub Combination kama vile PM, CM, CB nk. Walikuwa wanasoma na somo lingine lililokuwa linaitwa Education, halafu wanafanya mtihani wa form six kisha wanaongeza mwaka mmoja wanasoma Education Methodology halafu wanatoka Na Diploma ya Ualimu,ukifaulu sana baada ya kumaliza JKT ilikuwa unaunganisha University. Kwa hiyo walikuwa wanasoma miaka MITATU Na siyo minne. Lengo lilikuwa kupata waalimu bora wa sekondari Na vyuo vya ualimu.
 
Magu hakwenda JKT. Zamani walikuwa wakimaliza six,wanakwenda JKT then ndo chuo.
 
Hii mada haina heshima wala mashiko kutokana na aina ya uchangiaji.
Wachangiaji wengi mnazingua..
Hawa watoto waliosoma kipindi hiki unafaulu hata mzazi hashtuki *drs 7 wote wanafanya kuhamia sekondari* hawawezi kujua hii....zamani ukifaulu kwenda sekondari kijiji au mtaa wote unazizimaa na usipofanyiwa maombi au kupewa *missile* na babu yako kesho unakutwa ume - rest in peace.....by the way tulikuwa na *vijeba* na wale walituzidi umri sana tulikuwa tunaziita *njemba* zilikuwa zinapiga mkono na hata std 7 zaidi ya 4 ....sometimes watabe wa std 7 walikuwa wanakaa kikao cha dharura au kuomba assistance kutoka kitaa au shule ya jirani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwadanganya wenye akili zao ni ngumu sana.
Kwa uchambuzi ulioufanya, sio rahisi uncle kuwa aliweza kuingia primary akiwa na 8 yrs hasa ukizingia mfumo uliokuwa ukitumika kuwasajili darasa la kwanza (kuupitisha mkono wa kulia juu ya kichwa ili ushike sikio la kulia), jamii za wafugaji ambapo kipaumbele ilikuwa kuchunga ng'ombe.
Wenye taarifa za uhakika wataiweka sawa hii story
 
Hon. Kangi Alphaxard Lugola

Member Type : Constituent Member
Constituent : Mwibara
Political Party : CCM
Phone : +255759300805
P.O Box : P.O Box 486, Bunda
Email Address : a.lugola@bunge.go.tz
Date of Birth : 1963-05-23
 
mitihani ya form two ilianza mwaka 1985 Kangi alikuwa form two 1982 mtihani wa form two haukuwepo, pia by then sengerema walikuwa wanaenda best pupils, asingefeli
OK sawa
 
Usajili wa kutumia kupitisha mkono wa kulia kichwani uliishia mwanzoni kabisa mwa miaka ya sitini (1962-1963 ). Kuanzia mwaka 1964 mtindo huo haukutumika tena. Mimi mwenyewe nilianza darasa la kwanza 1965 nikiwa na miaka 8 tu wala sikusajiliwa kupitia utaratibu huo pamoja na wenzangu wote tulioasajiliwa darasa la kwanza mwaka huo. Hivyo mwaka 1967 alipoanza shule Mheshimiwa Magu utaratibu huo ulikuwa haupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima yako mkuu.
Mkuu, basi huko kwenu mlikuwa na bahati. Mimi nilifanya kulilia kwenda shule baada ya kuona wenzangu niliokuwa nacheza nao wameandikishwa halafu mi mkono haukufika sikioni.
Nilichonya siku ya pili nilitoroka nyumbani hadi shuleni. Nilikuwa na umbo dogo lkn nilikuwa na akili.
Walimu walipoona nalilia shule wakaniambia niandike jina langu. Nikaandika vizuri. Nikaambiwa nihesabu hadi kumi. Nikahesabu haraka sana. Nikaambiwe nihesabu kwa makumi hadi mia moja. Nikaweza. Yote hayo nilifundishwa na dada yangu home. Basi walipoona nimefanya vizuri nikaandikishwa. Miaka walinipunguzia, waliona kama naongeza miaka vile.
Nilianza la kwanza 1986.
 
Hivi unaweza kumfundisha uliemzidi miaka minne sekondari ?
Ndioo Kuna jamaa amesoma Lushoto Diploma ya Sheria akamaliza akaunga mzumbe Degree Mbeya campus alipomaliza akabaki kufundisha,wengine aliosoma nao diploma wakaenda kufanya kazi mahakamani walipotaka kujiendeleza wakamkuta mwanafunzi mwenzao wakiwa diploma Sasa ni mwl wao kwa level ya degree. Hiyo inawezekana kwa Magu pia kamaliza form six kaenda kufundisha sengerema na kumkuta kangi yupo form three au four
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…