Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

Kwa siku hizi ndiyo haiwezekani, lakini zaman ilikuwa mtu unaemzidi umri angeweza kuwa mwalim wako pia. Enzi hizo ilikuwa mwanafunzi wa miaka 18 anasoma darasa moja na mwanafunzi wa miaka 12.

Kumbuka JPM mzazi wake (baba) alikuwa ni mwalim so kuna uwezakano alisoma kwa umri mdogo nae Lugola alikuwa ni mtoto wa mkulima so alirudia shule mara kibao hachaguliwa kwenda secondary. Zamani ilikuwa ni kuchaguliwa kwenda secondary na siyo kushinda, kwa sababu ya uhaba wa shule. Enzi hizo kurudia shule hata mara nne ilikuwa ni jambo la kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika vyema hakuna cha kupunguza au kuongeza
 
Nimeshangazwa sana na maneno ya Rais Magufuli wakati akimtumbua Lugola kuwa aliwahi kuwa mwanafunzi wake Sengerema Secondary wakati nikimtazama Rais Magufuli na Lugola ni kama Lugola ni mzee kuliko Magu

sasa kwa wanaojua umri wa bwana Lugola wanifahamishe tafadhari

Nimeangalia kwenye tovuti ya bunge kuwa Lugola alisoma sengerema secondary kuanzia mwaka 1981-1984 labda uchunguzi rasmi uanzie hapo kuangalia wakati huo mkemia Magu alikuwa anapiga mzigo wapi

Haya maswali ni vigumu kupata majibu, kwani wengi wetu tunabuni/kukisia tu lakina hatuna majibu kamili. Wenye majibu ni hao wawili - LILIYEFUNDISHA NA ALIYEFUNDISHWA.
 
Cha ajabu hapo ni nini. Inawezekana Magufuli alimfundisha alivyokuwa amehitimu F6 utofauti wa age unaweza kuwa btn 2-6 yrs. Inawezekana pia Kangi aliingia shule umri ukiwa umeenda sana na hvyo kuwa sawa kiumri na Magu ama hata mkubwa kwa Magu. Nimefundisha wanafunzi wengi sana walio na umri sawa ama zaidi yangu hasa kipindi nimemaliza F6. Umri wake nenda Tovuti ya Bunge utaupata
 
Nimeshangazwa sana na maneno ya Rais Magufuli wakati akimtumbua Lugola kuwa aliwahi kuwa mwanafunzi wake Sengerema Secondary wakati nikimtazama Rais Magufuli na Lugola ni kama Lugola ni mzee kuliko Magu

sasa kwa wanaojua umri wa bwana Lugola wanifahamishe tafadhari

Nimeangalia kwenye tovuti ya bunge kuwa Lugola alisoma sengerema secondary kuanzia mwaka 1981-1984 labda uchunguzi rasmi uanzie hapo kuangalia wakati huo mkemia Magu alikuwa anapiga mzigo wapi
Ukitaka kujua tarehe ya kuzaliwa ya mtu yeyote maarufu mtafute kwa kutumia wikipedia. Hata hivyo inaonyesha kama Mwalimu Magufuli aliwahi kusoma, halafu Mh. Lugola akawa amechelewa kidogo, na hicho ndicho kilichosababisha wahusiane kama mwalimu na mwanafunzi wake. Kwa mfano, mimi mwaka 1993 nilikuwa nafundisha darasa la wanafunzi wa F3, baadhi yao walikuwa wananizidi umri, wakati huo nilikuwa tayari nimeshamaliza FVI na JKT nimetoka. Hata hivyo kwa kuwaangalia maumbo, wengine walikuwa wanaonekana kama ni wadogo kuliko mimi!
 
Hivi mtu mzima kama huyu kupenda kukata mauno kama kombeo mbele ya hadhara na raisi wake ni ukichaa, ushamba au uhayawani?
 
Secondary Jamani. Wewe secondary na Primary kulikuwa na mwalimu anaekuzidi miaka minne tu ?
Zamani huko iliwezekana sana, 2000 kurudi nyuma tulifundishwa na vijana waliomaliza A level na diploma, so ni rahisi sana ilikuwa ufundishwe na mtu kakuzidi 4-6yrs.
 
Magu siyo wa upe. Alimaliza Six mwaka 1981 .Mwaka huo huo akaanza chuo mkwawa. Najiuliza Dilpoma ya ualimu ilikuwa miaka mingapi ? Maana Kangi nae kaanza form one 1981 akamaliza 1984.
Pia kwa upande wa Magu kamaliza six Mkwawa high school na kusoma diploma hapo hapo.
Ina maana mkwawa ilikuwa secondary pia ilikuwa chuo cha diploma Ualimu ?
Duh, waliosoma MKWAWA HIGH SCHOOL miaka hiyo waliunganisha A level na Diploma, ilikuwa miaka mitatu kusoma A-level na Dip nadhani(kaka yangu alisomea hapo). Nikosolewe kama nimekosea...
 
Uhakiki muhimu, tusije kuingizwa chaka.

Mtu anayeanza form one na miaka 18 ubongo ushaanza kuwaza wanawake hapo napo kuna tatizo.
Wakati nimeanza form I nikiwa na miaka 14 wakati huo, kuna jamaa darasa moja walikuwa na miaka 18 hadi 24 na ndevu zao kabisa, tulisoma na baadhi ya wamasai walikuwa na zaidi ya miaka 25. Zamani hizo sio ajabu sana kusoma na vijeba
 
Nimeshangazwa sana na maneno ya Rais Magufuli wakati akimtumbua Lugola kuwa aliwahi kuwa mwanafunzi wake Sengerema Secondary wakati nikimtazama Rais Magufuli na Lugola ni kama Lugola ni mzee kuliko Magu

sasa kwa wanaojua umri wa bwana Lugola wanifahamishe tafadhari

Nimeangalia kwenye tovuti ya bunge kuwa Lugola alisoma sengerema secondary kuanzia mwaka 1981-1984 labda uchunguzi rasmi uanzie hapo kuangalia wakati huo mkemia Magu alikuwa anapiga mzigo wapi
Inawezekana alikuwa akisoma elimu ya watu wazima...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom