Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

[emoji23]lugola katumbuliwa ?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Basi Lugola alichelewa sana kuanza shule. Au alifeli la saba akarudia sana tena sana. Tatizo hawa wanasiasa utasikia tu wamesoma wapi na wapi ila miaka ipi hawasemi. Bashite nae haijulikani secondary alimaliza mwaka gani.
JPM amefundisha Sengerema sekondari mwaka 1983- 84. Akitokea chuo cha Ualimu Mkwawa.
 
Chuo kikuu,vyuoni huko sawa. Maana wengine wanatoka makazini. Secondary jamani ? ?????
miaka ile siyo kma sasa mathalani mm nmesoma pembezon mwa mji.. form 1 mm nlikua na miaka 16 na ndo nlikua mdgo kabisa wakati mkubwa alikua na 28, sijui hapa unapata picha??: zaman kuna waliochelewa kuanza shule especially miaka ya 80's kuna mzee hapa anakwambia kamaliza std 7 ana 24

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unaweza kumfundisha uliemzidi miaka minne sekondari ?

Mimi nadhani kwa kanda ya ziwa inawezekana, kama endapo Magu aliwahi kuanza kusoma na Kangi alichelewa,kwa maana miaka ya nyuma kanda ya ziwa kuna baadhi ya watu walikuwa wanachelewa sana kuanza shule.


Alexander
 
Magu 59.Alimfundisha vipi Lugola ?

Mbona kitu rahisi tu hapo kuelewa, kwa mfano mimi nina miaka 28 lakini naweza nikawa namfundisha mtu ambaye ana miaka 30. Kuwa mkubwa kiumri haikataivkuwa mwanafunzi kwa mwanafunzi kwake anayekuzidi umri. Kwa fani mwingine, Vyuo vikuu kuna vijana wamepata nafasi ya kuwa lecturers katika umri mdogo, kuna watu wenye umri mkubwa zaidi yao wanafundishwa nao. Kwahiyo m tu, suala la umri hata lisikupe tabu. Kangi ni mwanafunzi wa mzee Jpm na pia JPM pia ni mkubwa kiumri kwa Kangi


Happy dude [emoji67]‍[emoji538]
 
Kangi maana yake kengine(kitu kingine)
Lugola maana yake mtia aibu (mwenye kutia aibu)
Huyo jamaa ni msukuma nafikiri Mara ni wahamiaji tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana pia Magu hajazaliwa 1959, labda ni nyuma zaidi ya hapo
 
Nimeangalia kwenye tovuti ya bunge kuwa Lugola alisoma sengerema secondary kuanzia mwaka 1981-1984 labda uchunguzi rasmi uanzie hapo kuangalia wakati huo mkemia Magu alikuwa anapiga mzigo wapi

Alikuwa ni Mwalimu Sengerema Secondary.
 
Hivi unaweza kumfundisha uliemzidi miaka minne sekondari ?
Hapo kuna mawili, ni either mtumbuliwa alichelewa kuanza elimu au zamani kulikuwa na kautamaduni mtu akifeli darasa la saba anapewa jina la mwanafunzi mwingine pengine aliyekuwa darasa la 5 Ila hakuendelea na shule.
 
Nimeshangazwa sana na maneno ya Rais Magufuli wakati akimtumbua Lugola kuwa aliwahi kuwa mwanafunzi wake Sengerema Secondary wakati nikimtazama Rais Magufuli na Lugola ni kama Lugola ni mzee kuliko Magu

sasa kwa wanaojua umri wa bwana Lugola wanifahamishe tafadhari

Nimeangalia kwenye tovuti ya bunge kuwa Lugola alisoma sengerema secondary kuanzia mwaka 1981-1984 labda uchunguzi rasmi uanzie hapo kuangalia wakati huo mkemia Magu alikuwa anapiga mzigo wapi
wewe elewa moja kuwa kenge lugola kafundishwa na Rais. Ina maana huamini kauli ya Rais.!!!! Mbona una roho za kwa nini!?
 
Kwamba mtu wa 59 hawezi kumfundisha wa 64? Hivi mmeisahau Tanzania ya kabla ya MMEM na MMES! Kuna watu kwa bahati mbaya wanaotokea familia za wazazi wasio na mwanga wa elimu walikuwa wanasoma ni wakubwa sana. Mfano mimi wakati naenda kuanza drs la kwanza kuna mwamba alikuwa anaishi jirani yetu hana mpango kabisa wa kwenda shule maana alikuwa tayari ana hang out na washkaji flani wanafanya kazi kwenye mabasi flani kutoka wilayani kwetu kuja Mwanza. Ila mama yangu akawa kapambana akamuombea nafasi pale shuleni tukaanza nae. Bingwa alikuwa kijeba kweli kiasi kwamba kuna washkaji tuliwakuta drs la 7 ila walikuwa wakituonea tukashtaki kwa huyu mwamba anawpiga dizain hadi wanaruka madirishani wanakimbia. Imagine mtu wa drs la kwanza anampiga mtu wa drs la saba. Huyu mwamba alikuwa na umri gani jiulize. Sasa mfano dada yangu ambae mi naanza la kwanza yeye yuko la 5 angemaliza akaendelea na kuwa mwalimu asingeweza kuja kumfundisha huyu mwamba tuliekuwa nae japo kuwa sista angekuwa kamzidi kidogo au wamelingana na huyu jamaa? Zamani kulikuwa na watu wa ajabu mashuleni mtu mnasoma nae shule ya msingi ila wikend akienda kuchunga ng'ombe ndama akagongwa na nyoka au akapata shida yoyote jamaa anambeba ndama makumi ya kilomita kutoka alikokuwa anachungia hadi nyumbani, unajiuliza mtu wa hivi ana umri gani unabaki mdomo wazi
Huyo mwamba noma.
Msalimie sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom