Naomba kujua Bajeti inayotosha kutembelea Zanzibar

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Habari zenu ba ndugu

Nataka kwenda Zanzibar kukaa kama wiki na ubavu wa kushoto.
Kunahitaji bajeti kiasi gani kula, malazi, nauli na kutalii kidogo?

NB: Wananchi wa uchumi wa kati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda na elfu hamsini tu


Elfu ishirini vichwa viwili mnaenda ila wewe me utasaidia kutoa maji chini kule nyingine iliyobaki nunua mikate ya bofluro
 
Nauli 35,000 × 4 (kwenda na kurudi, kutoka Dar)...Business class.
Room 100,000 ×7 = 700,000
Nauli ndani ya Zenji 120,000 (7days)
Chakula + drinks 30,000 × 7
Viingilio si zaidi ya Tsh.20,000 per kichwa.

Hivyo andaa kama mil.moja hivi, hayo mengine yatajiadjust humohumo.
 
1. Download App inaitwa AirBnb
-hii itakusaidia kupata sehemu nzuri ya malazi kwa bei nafuu lets say price<25usd angalia mwenyewe sehem kali kwa bei ndogo zipo kibao mkuu usihangaike na sehem za laki sjui elf 80

2. Andaa nauli yako minimum 25,000 na maximum ni 80,000 hii ni kwenda tu na bei inategemea na class inayotaka wewe

3. Andaa pesa ya usafiri hasa kama utataka kwenda shamba ndio kuna starehe kwakua mpo wawili unaweza ukakodi gari IST ni 35,000 siku nzima

4. kwa upande wa chakula hapo unaweza kuestimate costs mwenyewe figures ninazoweka hapa chini ni kwa lunch and dinner tu na nimekadiria tu ila kwa kujibana kishkaji inaweza ikapungua au ikazidi
-maji 4000
-juice elf 8000
-chakula 25,000

nimekupa general overview kuhusu gharama utajua kwa kukadiria maelezo hapo juu
 
Hivi Zanzibar kuzuri?

Kwa wenzetu wazungu ambao wanakuja kwa ajili ya kujua historia, kunaweza kuwa kuzuri, ila kwa sisi wabongo ni ngumu kuuon uzuri wake.

Nimeshajaribu kuzungukia maeneo mengi ili niuone uzuri wa Zanzibar, aisee nimeshindwa. Ila utakuta wazungu wamejaa na wanainjoi kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…