Naomba kujua gharama za kuweka tiles kwa chumba kimoja

Hizi mnazouliza hapa ni hesabu za Std 6 wakuu, hakuna utaalam sana hapa. Ni unachukua "Eneo" la chumba kizima unagawanya kwa "eneo" la tile moja ili upate zitahitajika tiles ngapi kujaza hicho chumba.

Sasa tiles mara nyingi haziuzwi moja moja bali kwa mafungu (box) hivyo unachukua idadi ya tiles zinazohitajika kujaza chumba unagawa kwa idadi ya tiles zinazokaa kwenye kila boksi upate ni maboksi mangapi.

NB
Eneo = Urefu x Upana
 
Mfano,
1) Umepima Chumba ukapata urefu ni futi 10 na upana ni futi 10. Badili hivi vipimo viwe katika meter inakua urefu mita 3 na upana mita 3.

Eneo la chumba = Urefu x Upana,
= mita 3 x mita 3,
= mita za eneo 9.

2) Labda tile moja ina urefu wa sentimeta 40 na upana huo huo. Badili napo hivi vipimo kua katika mita. Hapo itakuani 0.4mita urefu na upana.
Eneo la tile moja = 0.4mita x 0.4mita
=mita za eneo 0.16

Kwa hiyo chumba chenye mita za eneo 9 pale juu (1) kitatumia tiles zenye mita za eneo 0.16 kila moja pale juu (2) zipatazo 9÷0.16 =56.25.

Na kama tiles hizo utazikuta zimefungwa kwenye maboksi ya tiles sita sita kila boksi labda basi yatahitajika maboksi 56.25÷6 = 9.375 kuweza kujaza hicho chumba. Sasa sababu boksi zinauzwa nzima nzima basi kadirio linakua la kuongeza hivyo boksi 10 zitahitajika hapo.
 
Hesabu hizi hapo juu zinaweza kubadilika kulingana na yafuatayo ambayo nimeweka kama mfano tu.
1) Chumba chako sio futi 10 x futi 10
2) Tiles unazotumia sio sentimeta 40 kila upande
3) Kwenye boksi hazikai tiles 6.

NB
Mimi sio fundi na sina utaalam wowote huko, nimeandika tu katika context ya ki hesabu zaidi.
 
Jibu zuri la kiufundi ubarikiwe sana
 
Uko vizuri mkuu umenipa somo sana
 
Na bei za mafundi mnasema ni estimate TZS 5,000/- Kwa Square meter, wapo humu hao mafundi?
 
Umeupiga mwingi. Kongore kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii comment imefanya nikudharau
Nafatilia comment za watu napata kuwapima vichwani mwao.

Ikumbukwe hii platform ina watu wachache. Na hawa wachache ni wale tunaokubaliana sote kwamba wengi ni Elites na wa ajielewa ndio maana wako humu.

Lakini kama uwezo wao uko hivi kwa vitu vidogo namna hii vya Square metres na Imagine wale ambao hawako humu( low minded class) watakuwa na hali gani.

Katiba Mpya haitapatikana kamwe😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…