Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nime search sijaona
Ndugu yangu mimi nina swali . Pamoja na urusi kusifiwa sana kuwa iko strong kiuchumi . Kijeshi. Maliasili . Technology na mambo mengi ........ila sijawahi kusikia urusi imetoa misaada labda kwenye tsunami . Kupokea wakimbizi. Kwenye njaa au maafa mengine yote tofauti na nchi kama UK. France. Italy. Germany. ........hata Greece yanye njaa inapokea wakimbizi ..... Nikiisikia urusi basi ni kwenye vita. Na hata nyumbani sijaona NGO yeyote ya urusi zaidi ya culture center yao ya kufundishia lugha..........au ndio bado inajipigia debe au mnaipigia debe kama enzi zile. Nashauri urusi na nyie wapiga debe wake muache. Urusi haiko hivyo unavyotaka tuamini. Uchumi mkubwa wa urusi unategemea gas. Na hivi sasa mafuta yameshuka bei duniani. Urusi kuna njaa na hela yao inazidi kuporomoka thamani. Kifupi urusi ni mbishi tuHeri ya mwaka mpya ndugu zangu,
Nlikuwa nasheherehekea mwaka mpya pamoja na familia ndiyo maana nikawa adimu humu.
Lakini EPISODE FOUR nadhani leo usiku au jioni nitaipost
Aisee ngoja nisogee karibu na chuo nijiunge ili niwe na MB za kutosha kwa ajili ya epsode 4.Heri ya mwaka mpya ndugu zangu,
Nlikuwa nasheherehekea mwaka mpya pamoja na familia ndiyo maana nikawa adimu humu.
Lakini EPISODE FOUR nadhani leo usiku au jioni nitaipost
Mkuu urusi kuna njaa? Embu tupe link tujiridhishe.. Na labda wakati unatafuta hiyo link jaribu pia kupitia idadi ya wahamiajia wanaoenda kutafuta kazi urusi kutokea nchi zinazozunguka urusi.. Angalia pia hizo link kujua pato la mwaka la Urusi.. Pitia pia mauzo ya bidhaa za Urusi (ukitoa mafuta na gesi).. Pitia pia idadi ya watalii wanaotoka urusi kila mwaka kwenda nchi kama Misri na Uturuki (kwa mtizamo wangu mimi mdogo tu huwezi kupeleka mamilioni ya watalii nje kama nchi yako hata kujilisha haiwezi)Ndugu yangu mimi nina swali . Pamoja na urusi kusifiwa sana kuwa iko strong kiuchumi . Kijeshi. Maliasili . Technology na mambo mengi ........ila sijawahi kusikia urusi imetoa misaada labda kwenye tsunami . Kupokea wakimbizi. Kwenye njaa au maafa mengine yote tofauti na nchi kama UK. France. Italy. Germany. ........hata Greece yanye njaa inapokea wakimbizi ..... Nikiisikia urusi basi ni kwenye vita. Na hata nyumbani sijaona NGO yeyote ya urusi zaidi ya culture center yao ya kufundishia lugha..........au ndio bado inajipigia debe au mnaipigia debe kama enzi zile. Nashauri urusi na nyie wapiga debe wake muache. Urusi haiko hivyo unavyotaka tuamini. Uchumi mkubwa wa urusi unategemea gas. Na hivi sasa mafuta yameshuka bei duniani. Urusi kuna njaa na hela yao inazidi kuporomoka thamani. Kifupi urusi ni mbishi tu
Kutalii ni hobbie ........wa US wengi hawatoki nje ya nchi yao.....baadhi ya nchi zilizoizunguka russia ndio masikini mfano romania .....tuachane na uchumi wa kwenye makaratasi huwezi fananisha russia na western europe au US in any how.....tafuta mtu aliyetembelea nchi zote hizo mbili awe mkweli tu.Mkuu urusi kuna njaa? Embu tupe link tujiridhishe.. Na labda wakati unatafuta hiyo link jaribu pia kupitia idadi ya wahamiajia wanaoenda kutafuta kazi urusi kutokea nchi zinazozunguka urusi.. Angalia pia hizo link kujua pato la mwaka la Urusi.. Pitia pia mauzo ya bidhaa za Urusi (ukitoa mafuta na gesi).. Pitia pia idadi ya watalii wanaotoka urusi kila mwaka kwenda nchi kama Misri na Uturuki (kwa mtizamo wangu mimi mdogo tu huwezi kupeleka mamilioni ya watalii nje kama nchi yako hata kujilisha haiwezi)
Nani alijua kama Greece,Romania,Egypty, UK,Roma, uyunani,zingepotea,so nimuda Tuuu ndio utakaoamua kwa USA kuanguka
An expensive hobby i must agree… hakuna popote mtu kasema chumi zinafanana swali lilikuwa kama kweli warusi wana njaa utujuze hivyo vyanzo vya habari. Kuhusu kutafuta mtu aliyetembela huko hamna haja nimeshafika nami…Kutalii ni hobbie ........wa US wengi hawatoki nje ya nchi yao.....baadhi ya nchi zilizoizunguka russia ndio masikini mfano romania .....tuachane na uchumi wa kwenye makaratasi huwezi fananisha russia na western europe au US in any how.....tafuta mtu aliyetembelea nchi zote hizo mbili awe mkweli tu.
Ndugu yangu mimi nina swali . Pamoja na urusi kusifiwa sana kuwa iko strong kiuchumi . Kijeshi. Maliasili . Technology na mambo mengi ........ila sijawahi kusikia urusi imetoa misaada labda kwenye tsunami . Kupokea wakimbizi. Kwenye njaa au maafa mengine yote tofauti na nchi kama UK. France. Italy. Germany. ........hata Greece yanye njaa inapokea wakimbizi ..... Nikiisikia urusi basi ni kwenye vita. Na hata nyumbani sijaona NGO yeyote ya urusi zaidi ya culture center yao ya kufundishia lugha..........au ndio bado inajipigia debe au mnaipigia debe kama enzi zile. Nashauri urusi na nyie wapiga debe wake muache. Urusi haiko hivyo unavyotaka tuamini. Uchumi mkubwa wa urusi unategemea gas. Na hivi sasa mafuta yameshuka bei duniani. Urusi kuna njaa na hela yao inazidi kuporomoka thamani. Kifupi urusi ni mbishi tu
The legend himself vladmir putinSiku ambayo huyu rais wa urusi wa sasa Vladimir Vladimorovich Putin akifa wamarekani na washirika wao watafanya sphere he. Ni umiza kichwa kwao sana, namkubali sana huyu jamaa
COLD WAR: PHASE 4- The New Deal, Roosevelt and Ascendancy of America.
Baada ya dunia kupata mtikisiko wa kiuchumi mwaka 1929 taifa la Marekani lilikuwa kwenye mkanganyiko mkubwa kutokana na kutopangilia uchumi wake vizuri. Mwaka 1932 uchaguzi mkuu ulifanyika Marekani na raisi mpya alipatikana. Huyu ni Franklin Delano Roosevelt na makamu wake wa raisi alikuwa anaitwa Harry S Truman,walitoka katika chama cha Democrat. Harry S Truman ni maarufu sana kwasababu ndiye aliyeangusha mabomu ya kiatomiki huko Japan;pia sera zake zilichochea Vita Baridi (COLD WAR)
Ikumbukwe huyu Roosevelt alikuwa anatembelea kwenye kiti cha kusukuma kwa mataili wazungu wanaita (Wheel Chair). Hii ilitokana na kupata ugonjwa wa kupooza (paralysis) uliosababishwa na Polio.
Sasa bwana Roosevelt kaingia madarakani na nchi iko kwenye hari mbaya kiuchumi; mwaka 1933 alivyokuwa anaapishwa alisema kwa Wamarekani kwamba "I pledge myself and this country to the New Deal, and may God help me" na tena akawaambia Wamarekani "The only thing to fear is fear itself" . Hii new Deal ilikuwa ni sera ya kiuchumi ambayo raisi Roosevelt aliipitisha ili kuweza kukuza uchumi kwa kasi.
Kisheria hii sera ya kiuchumi ilitaka raisi aongezewe madaraka zaidi ili aweze kufanya mambo ya msingi bila kuzuiwa. Hii ilizua mjadala ndani ya Bunge la Marekani kwasababu Republicans walipinga sana wakasema raisi atakuwa kama mfalme kitu ambacho kitahatarisha misingi ya taifa la Marekani.
Lakini UMMA wa watu wa Marekani uliwaamini Democrats kwasababu Uchumi wa Marekani uliharibikia mikononi mwa Republicans, hivyo THE NEW DEAL ikapita.
Kitu cha kukumbuka ni kwamba katika historia ya Marekani hakuna raisi ambaye amewahi kukaa madarakani kwa muda mrefu kama Franklin Delano Roosevelt. Alikaa madarakani kwa miaka 15 na alifia ofisini. Marekani ya leo ambayo ni taifa kubwa lenye ushawishi mkubwa kisiasa, kielimu, kitamaduni, kidiplomasia, kiuchumi na kijeshi lilijengwa na Roosevelt pamoja na New Deal Program.
The New Deal framework yake ilipitisha baadhi ya sheria ambazo ziliweza kutengeneza taifa la wafanyakazi, kuanzia watoto hadi wakubwa. Kila mtu ndani ya nchi mwenye uwezo wa kufanya kazi alifanya kazi.
Sasa yafuatayo ni matukio muhimu ndani ya new deal.
1. The NIRA- National Industrial Recovery Act.
Sheria hii ililenga kuinua uchumi wa viwanda ambavyo vulikuwa vimefuka na vinavyokaribia kufa ndani ya Marekani. Kwanza serikali iliwaajiri watu wengi hasa vijana kufanya kazi katika miradi mingi ya serikali kama ujenzi wa barabara, majengo, hospitali, madaraja na mabwawa. Hili lilisaidia kupunguza tatizo la ajira ndani ya Marekani. Pili serikali ilisimamia uzalishaji katika viwanda binafsi ili kusaidia mambo kama fair competition, kuzuia unnecessary overproduction na kulinda maslahi ya wafanyakazi wa viwanda.
Mpango huu ulizaa matunda mengi na hasa wakati wa vita ya pili ya dunia viwanda vya Marekani vilikuwa na nguvu kazi ya kutosha; hivyo kumfanya Marekani auze silaha kwa pande zote mbili zilizokuwa zinapigana.(The Allies Vs The Axis)
2. The TVA- The Tennessee Valley Authority Act.
Kama nilivyosema kwenye nyaraka zilizopita kwamba sababu moja ya kuanguka kwa uchumi wa Marekani ilikuwa ni Ukame. Sasa serikali ya Delano Roosevelt ilianza kufanya project mbali mbali ili kuondoa tatizo la ukame. Ikumbukwe ukame ulisababisha kuanguka kwa kilimo, viwanda vya umeme na upungufu wa chakula kwasababu mbali na viwanda Marekani inategemea sana kilimo.
Wakaanza kujenga mabwawa makubwa ili kuzalisha umeme na kutanua kilimo cha umwagiliaji.
Pia walikuwa wanatengeneza pembejeo za kilimo kama mbole ya bei ndogo kwa wakulima ili waweze kuongeza kasi ya uzalishaji; walianza kampeni ya kupanda miti; kuzuia mafuriko na mmomonyoko wa udongo; waliimarisha uvuvi wa ndani; waliimarisha usafiri wa njia ya maji na zaidi walipewa kazi ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
3. The Agriculture Adjustment Act.
Sheria hii ilisaidia kuwainua wakulima kwa kuwaambia wazalishe kidogo ili kuimarisha bei za mazao yao.
Mbali na mazao kuwa na bei nzuri, wakulima walikuwa wanalipwa kiasi kingine cha pesa kama fidia ya kupunguza uzalishaji.
Pia wakulima walisaidiwa kupewa mikopo na bei za mazao zikisimamiwa vizuri na serikali; serikali mnamo mwaka 1936 ilisema wakulima wapande mazao yanayozui mmonyoko wa udongo ili kuzui majanga mengi kwenye kilimo yasiwepo.
4. The Emergency Banking Act.
Hii ilipitishwa kwa ajili ya kuzisaidia benki za marekani.
Kwanza raisi alitangaza BANK HOLIDAY, ili benki zote zifungwe ndani ya siku nne ili ukaguzi ufanyike na serikali ijue ni benki zipi zilikuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Baada ya siku nne benki zilizokuwa na uwezo wa kufanya kazi zilifunguliwa na kuwekwa chini ya uangalizi mkubwa wa serikali.
Hili lilisaidia kurudisha imani ya wawekezaji kwasababu kipindi cha anguko la kiuchumi watu wengi walitoa pesa zao katika mabenki hivyo kusababisha financial system ya nchi nzima kukwama.
5. Formation of the Civilian Conservation Corps.
Hili lilisaidia kuanzisha ajira zaidi ya laki mbili na hamsini kwa watu wasio na ajira; watu walitakiwa wapande miti na kutunza mazingira kwa ujumla ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.
6. The Labour Relations Act.
Hii ilipanga kuwalinda wafanyaki wa viwandani hasa kipindi hichi cha mtikisiko ambapo watu wanaweza wakawa wananyonywa bila sababu halafu wenye viwanda wanapata faida.
Basi serikali ilipanga masaa ya kufanya kazi na mishahara ambayo inabidi wafanyakazi wapewe.
Mazingira ya kufanyia kazi yakaboreshwa ili kulinda afya na uhai wa wafanyakazi.
Serikali ilipiga marufuku Child labour,watoto chini ya miaka kumi na sita walitakiwa wasifanye kazi zozote za viwandani wala migodini.
Na kama watafanya basi wapewe kazi nyepesi ambazo hazitaathiri afya na makuzi yao ya kielimu.
Hivyo basi watoto nao wakawa wanafanya kazi baada ya kutoka shule na kulipwa mishahara yao mizuri tu.
7. Reduction of Government Spending.
Serikali ya marekani ilikata matumizi yasiyo na maana kwa mda huo. Japo wamarekani wengi walikosoa hili jambo lakini kwa wakatin ule ilibidi kila mtu ajitoe kwa ajili ya nchi yake.
Mishahara kwa wafanyakazi waliostaafu na wale wa Umma ambayo ilikuwa kwenye mfumo wa malipo ilipelekwa kwingine. Ambapo serikali ilichukua kiasi cha Dollar za Marekani Millioni 500 kwa ajili ya kazi nyingine za haraka.
8. 100 days Congress Holiday.
Bunge la marekani baada ya kupitisha sheria ilibidi lisitishe kazi zake kwa muda wa siku mia moja ili kupinguza matumizi na kwenda kusimamia shughuli za maendeleo kwa ufanisi katika majimbo yao.
Hili lilisaidia sana miradi ya kazi kwenda vizuri na kupata mwelekeo mpya kwasababu kila kiongozi alikuwa anawajibika na majukumu yale makubwa ya bunge alipewa raisi Roosevelt.
Mambo aliyofanya Roosevelt ni mengi na hatuwezi kuyamaliza katika hii episode kwasbabu mwelekeo Wetu ni kwenye Cold War.
Haya na sasa huko Ulaya Mnamo mwaka 1933 naye Hitler akaupata Uwaziri mkuu(Chancellor) na Uraisi wa Ujerumani. Hili nitalielezea katika episode ya tano.
Ila ikumbukwe New Deal ni sera iliyolisaidia taifa la Marekani hadi mnamo miaka ya 1936 Marekani alikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao ya chakula na nafaka kwa mataifa ya ulaya.
Pia hadi vita ya pili inaanza mwaka 1939 Marekani hakuchagua upande wowote akawa(A NEUTRAL STATE), alifanya biashara kubwa sana ya silaha za vita rekodi ambayo haijavunjwa mpaka leo.
Kwa kifupi hadi kufika mwaka 1933 Marekani alikuwa anazalisha silaha za kivita nyingi zaidi ya Mjerumani, Italy, Spain na Japani. Kitu kilichomnyima raha sana Adolf Hitler na Joseph Stalin.
Wanasayansi wengi wa Ujerumani walitorokea Marekani ambapo ilikuwa ndiyo the NEW BEACON OF DEMOCRACY and GOOD GOVERNANCE in the world.
Waliogopa kwenda Urusi kwasababu ya Ukomunisti na mifumo ya kidikteta ya Joseph Stalin ambayo ilikuwa inaua watu ambao iliwadhania ni tishia kwa usalama wa USSR.
Wakina Elbert Einstein na wanasayansi wngine waliingia Marekani na kumueleza raisi Roosevelt juu ya mipango ya Hitler ya kutengeneza silaha za maangamizi ambazo zingeweza kubadilisha wimbi la vita kwa Ujerumani. Kipindi hichi Ujerumani walikuwa wamebanwa kwenye kona baada ya kupigwa vibaya na Mrusi mwaka 1941 kakita vita inayoitwa THE GREAT PATRIOTIC WAR or THE BATTLE FOR STALINGRAD.
Warusi zaidi ya milioni 26 walikufa sasa wakawa wanataka kulipiza kisasai na pia mwaka huo wa 1941 Marekani alijiingiza kwenye vita rasmi baada ya Mjapani kuliupua visiwa vya Marekani vya Hawaii.
Mbali na hapo Marekani alikuwa naogopa kwamba asipoingia vitani Mjerumani akashinda basi hata mikopa aliyotoa kwa matifa ya ulaya haitalipwa kwasababu Hitler aliapa kwenda Marekani baada ya Ulaya.
Vivyo hivyo Hitler aligoma kulipa madeni ya Uingereza na Ufaransa mnamo mwaka 1933 na kuitoa Ujerumani kwenye the League of Nations ili wajipange kutawala dunia.
Marekani alipewa siri nyingi za kijeshi za Mjerumani kwasababu ndilo taifa lilokuwa na rekodi ya kuwa na technolojia kubwa ya kijeshi REKODI AMBAYO MAREKANI NA URUSI hawajaivunja kwa miaka yao zaidi ya 60's baada ya vita ya dunia. Wataalamu wa mambo ya Vita, national geographic na hata MIT wamekubali kwamba teknolojia ya Ujerumani ilikuwa miaka 10 kama siyo ishirini mbele ya teknolojia ya mataifa yote ya dunia.
- Ujerumani ndiye mwanzilishi wa Modern Rocket science,
- alianza kufanya atomic energy experiment hata kabla ya dunia kujua,
- ndiye mwanzilishi wa stealth technology kwenye ndege,
- ndiye wa kwanza kuanzisha experiment ya Super soldier ambapo mwaka 1945 alifanikiwa kutengeza vidonge vya kuongeza nguvu na wanajeshi waliojaribiwa waliweza kwenda maili 20 bila kupumzika (sema wengi walikufa kwa side effects),
- idea ya kuwa na space station na satellites Mrusia aliikuta berlin,
- Drone ya kwanza ilikutwa Berlin sema ilikuwa haijamalizika,
- Experiment nyingi kuhusu mwili wa binadamu zilifanywa na Daktari katili wa Ujerumani anayeitwa Joseph Mengele ambapo alikuwa anawafanyia wayahudi,
- Submarine za kisasa zilitoa idea nyingi ujerumani kwenye Submarine zake zilizoitwa U-Boat au kijerumani ni Untersee boot( undersea boat)
- Magari ya Ujerumani yaliweza kwenda muda mrefu bila mafuta mengi.
- Upelelezi wa Phone tapping umeanzishwa na Shirika la kijasusi la ujerumani la ABHWER.
- Vita ya kisaikolojia, media manipulation and propaganda machinery vilianzishwa na waziri wa propaganda wa Ujerumani anayeitwa Joseph Goebbels. C.I.A na K.G.B walizitumia mbinu zake katika vita baridi. Fuatilia CIA operation inaitwa Mockingbird ndiyo utajua jinsi intellijensia zinavyocheza na media.
Kwa kifupi haya yote utayapata kwenye
- Cambridge Encyclopedia of War.
- Encyclopedia of Modern Warfare.
- Encyclopedia of Espionage and Intelligence.
- Encyclopedia of the CIA.
- Encyclopedia of Modern Propaganda.
- The Truman Diary
- Cambridge History of the Cold War.
Ambapo watalaam wa historia wanakwambia mpaka mwaka 1914 Mwingereza alikuwa na Wanasayansi kama 6000, Marekani alikuwa na wanasayansi kama wasiozidi 20000 na Mjerumani pekee alikuwa na wanasayansi 600000.
Rekodi kubwa sana kwa kipindi hicho na ilikuwa ni dalili ya kuwekeza sana kwenye elimu na uzalendo.
Hadi vita ya pili ya dunia inaisha Marekani pekee alirecruit wanasayansi zaid ya 1500 wa Ujerumani kwa kuwatishia kama wasipokubali atawapeleka NUREMBERG TRIBUNAL ambayo ilikuwa ni mahakama ya uhalifu wa kivita miaka ya 1945.
Miaka ya 1930's wanasayansi wa Ujerumani na Einstein akiwemo walianzisha THE MANHATTAN PROJECT kwa ajili ya kutengeneza silaha za kiatomiki ili kumaliza vita ya dunia na Kuwatishia Wakomunisti.
Hili lilifanywa kwa suri mkubwa sana lakini hadi Roosevelt anakufa mwaka 1945 makamu wake anaapishwa kuwa raisi alikuwa hajui uwepo wa hiyo Project.
Jambo la kifurahisha ni kwamba Stalin na NKVD ambalo ni shirika la kijasusi la Urusi walikuwa wanajua uwepo wa silaha hizo na wakapandikiza wanasayansi ambao walikuja kuuza siri hizo kwa Mrusi.
Yote haya nitaongelea kwenye episode ya 6.
End of Episode 4 stay tunned for episode 5
Umesomeka mkuu salute kwa kuingia chimbo kutujia na hizi nondo.. Somewhere katika episode zako zijazo naomba kufahamu kiasi cha ushiriki wa Urusi kwenye vita ya Korea ya 1950-1953 ambapo naambiwa zaidi ya wanajeshi elfu hamsini wa Marekani walikufa@Tibet , @Paw , @Necha Lauwo , @gwijimimi , @cognition , @Kabaunyeri , @Mkereketwa_Huyu , @mmmkme , @Ramark , @Erijo , @mkamangi2 , @mtembea kwa miguu , @Gide MK , @semper saratoga , @Chakochangu , @Mwamba028 , @born again pagan , @k_dizle , @OME123 , @kagombe , @jay-millions , @JOSEPH LUHUSA , @WhySoSerious , @MeinKempf , @Nando , @pikachu
Episode 4 Tayari.