Naomba kujua idadi ya Madarasa yaliyojengwa wilayani Ngorongoro mwaka 2021/2022. Baada ya hapo mtajua mwekekeo

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Hali wadau wa JF, habari zenu.

Naomba kujua idadi ya Madarasa yaliyojengwa huko wilayani Ngorongoro. Ni kwa upande wa elimu ya Msingi na secondary.

Ikumbukwe hivi Sasa Kuna fukuto la kuwahamisha wananchi wa huko kwenda maeneo mengine. Lengo ni kuokoa hifadhi ya Crater ya Ngorongoro.

Lengo langu hasa ni kutaka kujua Kama tetesi hizi ni kweli. Ikiwa Madarsa mengi yamejengwa mwaka 2021/2022 basi huu ni uzushi. Kama hayakujengwa basi huu mpango wa kuwaondoa wakazi hao ulikuwapo tangu mwanzo.

Naomba tujadili takwimu za madarasa na maendeleo mengine. Kuhamishwa tuiache kwa sababu nyuzi zipo humu.

Asanteni nyote na karibuni.
 
Freed Freed
Takwimu unazohitaji ni za wilaya nzima ya Ngorongoro au unahitaji takwimu kwenye zile kata na vijiji vilivyo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi??
(Jaribu kurekebisha swali lako ili majibu yawe na uhalisia)
 
Na bahati mbaya zaidi yale madarasa yalijengwa bila kuwekewa matairi.

Yangekuwa na matairi ingekuwa rahisi kuyasukuma kuelekea kule watakapohamishiwa akina Yero Maasai wa FM Academia.
 
Wengi wanajua wilaya nzima ya ngorongoro ni hifadhi. Tafadhali ieleweke eneo la bonde la hifadhi ni kisehemu kidogo tu ya wilaya nzima ambayo makao makuu ni loliondo kule kwa babu wa samunge.
 
Kimsingi maeneo mengi yenye utata hasa karibu na protected areas mashule hayajajengwa....kulikuwa ma vijiji takiribani 940 venye mgogoro na hifadhi mbalimbali....kwa kauli ya Magufuli vingi vilireheshewa ardhi, lakini baadhi bado.

Baadhi vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Riaha haviruhusiwi kujenga shule...hata huu mgao wa juzi haukuwepo.

Kuna kata moja wanadai pesa imeliwa ila hiyo nadhani wanapoteza watu tu!!
 
Hapo sasa
 
Na bahati mbaya zaidi yale madarasa yalijengwa bila kuwekewa matairi.

Yangekuwa na matairi ingekuwa rahisi kuyasukuma kuelekea kule watakapohamishiwa akina Yero Maasai wa FM Academia.
Sasa serikali inajengaje miundombinu na muda mfupi baadae kuanzisha mjadala wa kuwahamisha watu maeneo hayo?
 
Freed Freed
Takwimu unazohitaji ni za wilaya nzima ya Ngorongoro au unahitaji takwimu kwenye zile kata na vijiji vilivyo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi??
(Jaribu kurekebisha swali lako ili majibu yawe na uhalisia)
Mimi nilijua wilaya nzima inahamishwa na halmashauri kufutwa. Sina ufahamu Sana. Nafuatilia vyombo vya habari tu.
 
Hapana Mkuu...
Wilaya ya Ngorongoro ina tarafa 3 na kata kama 21 hivi.
Makao makuu yapo Loliondo, kama 180KM, masaa 4 hivi kutoka yalipo makao makuu ya NCAA.
Karibia nusu yote ya wilaya upande wa kusini inadondokea ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Hivyo ni sawa kusema kuwa nusu ya wilaya ipo ndani ya hifadhi na nusu nyingine ipo nje.
Hiyo nusu iliyo ndani ya hifadhi ina jumla ya kata 11 na vijiji kama 25 hivi.
Na matumizi ya hiyo nusu ndiyo chanzo cha mgogoro huu mnaohusikia kwa sasa (japo ni maarufu kwa takribani miaka 20 na zaidi).
Mle ndani shughuli za kawaida za wenyeji zinaruhusiwa isipokuwa uwindaji, kilimo na ujenzi wa makazi ya kudumu (concrete) ili kulinda na kuendeleza hadhi ya hifadhi. Wenyeji wana huduma mbali mbali za kijamii na kwa miaka mingi NCAA inawashurutisha kuishi maisha ya kuwa kitega uchumi cha utalii kwa kuanzisha "Kanjiro" (cultural centres/bomas).
Viongozi wa wilaya, tarafa, kata na vijiji vilivyomo ndani ya NCA wanajumuishwa kwa pamoja kwenye Baraza la Wafugaji (NPC) lenye wajumbe 72. Baraza limekasimiwa majukumu ya kuratibu ushirikiano na NCAA ili kutekeleza malengo mtambuka ya NCA.
Centres maarufu zinazo ibuka kwa kasi ndani ya NCA ni Kakesio, Endulen, Nainokanoka, Olchaniomelok, Kimba, Makao, Alailelai kutaja kwa uchache.
Nje ya hifadhi upande wa kaskazini zaidi kuna pori la loliondo ambako shughuli zote zinaruhusiwa kama kawaida.
Japo napo wenyeji wanakabiliana na makucha ya wawindaji katili wa kiarabu (OBC) waliomilikishwa pori lote la Loliondo.
Kifupi mgogoro wa wenyeji wa Ngorongoro na serikali ni mgogoro mkubwa sana.
Na una athari zake kwenye uhifadhi na biadhara ya utalii.
Yapo mengi ya kueleza lakini kwa kuwa ulielekeza kuwa kuna nyuzi nyingi kuhusu hili sakata la Ngorongoro naomba kuishia hapa.
Nimeona nirahisishwe kwa hayo maelezo ili walio na takwimu wajikite maeneo yaliyo ndani ya NCA na si wilaya nzima ya Ngorongoro. Make ndipo penye mgogoro huu wa sasa.

Nawasilisha. 🙏🙏🙏

NB:
1. NCA - Ngorongoro Conservation Area (maeneo yaliyo ndani ya mipaka ya hifadhi)
2. NCAA - Ngorongoro Conservation Area Authority (Mamlaka inayosimamia hifadhi)
3. OBC - Otterlo Bussiness Corporation (Kampuni binafsi ya utalii wa kiwandaji ya mwanamfalme wa Uarabuni)
4. NPC - Ngorongoro Pastoral Council (Baraza la Wafugaji)
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri. Je hilo eneo la NCA, shule na taasisi nyingine zimeboreshwa 21/22?
 
Back
Top Bottom