Mimi nilijua wilaya nzima inahamishwa na halmashauri kufutwa. Sina ufahamu Sana. Nafuatilia vyombo vya habari tu.
Hapana Mkuu...
Wilaya ya Ngorongoro ina tarafa 3 na kata kama 21 hivi.
Makao makuu yapo Loliondo, kama 180KM, masaa 4 hivi kutoka yalipo makao makuu ya NCAA.
Karibia nusu yote ya wilaya upande wa kusini inadondokea ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Hivyo ni sawa kusema kuwa nusu ya wilaya ipo ndani ya hifadhi na nusu nyingine ipo nje.
Hiyo nusu iliyo ndani ya hifadhi ina jumla ya kata 11 na vijiji kama 25 hivi.
Na matumizi ya hiyo nusu ndiyo chanzo cha mgogoro huu mnaohusikia kwa sasa (japo ni maarufu kwa takribani miaka 20 na zaidi).
Mle ndani shughuli za kawaida za wenyeji zinaruhusiwa isipokuwa uwindaji, kilimo na ujenzi wa makazi ya kudumu (concrete) ili kulinda na kuendeleza hadhi ya hifadhi. Wenyeji wana huduma mbali mbali za kijamii na kwa miaka mingi NCAA inawashurutisha kuishi maisha ya kuwa kitega uchumi cha utalii kwa kuanzisha "Kanjiro" (cultural centres/bomas).
Viongozi wa wilaya, tarafa, kata na vijiji vilivyomo ndani ya NCA wanajumuishwa kwa pamoja kwenye Baraza la Wafugaji (NPC) lenye wajumbe 72. Baraza limekasimiwa majukumu ya kuratibu ushirikiano na NCAA ili kutekeleza malengo mtambuka ya NCA.
Centres maarufu zinazo ibuka kwa kasi ndani ya NCA ni Kakesio, Endulen, Nainokanoka, Olchaniomelok, Kimba, Makao, Alailelai kutaja kwa uchache.
Nje ya hifadhi upande wa kaskazini zaidi kuna pori la loliondo ambako shughuli zote zinaruhusiwa kama kawaida.
Japo napo wenyeji wanakabiliana na makucha ya wawindaji katili wa kiarabu (OBC) waliomilikishwa pori lote la Loliondo.
Kifupi mgogoro wa wenyeji wa Ngorongoro na serikali ni mgogoro mkubwa sana.
Na una athari zake kwenye uhifadhi na biadhara ya utalii.
Yapo mengi ya kueleza lakini kwa kuwa ulielekeza kuwa kuna nyuzi nyingi kuhusu hili sakata la Ngorongoro naomba kuishia hapa.
Nimeona nirahisishwe kwa hayo maelezo ili walio na takwimu wajikite maeneo yaliyo ndani ya NCA na si wilaya nzima ya Ngorongoro. Make ndipo penye mgogoro huu wa sasa.
Nawasilisha. πππ
NB:
1. NCA - Ngorongoro Conservation Area (maeneo yaliyo ndani ya mipaka ya hifadhi)
2. NCAA - Ngorongoro Conservation Area Authority (Mamlaka inayosimamia hifadhi)
3. OBC - Otterlo Bussiness Corporation (Kampuni binafsi ya utalii wa kiwandaji ya mwanamfalme wa Uarabuni)
4. NPC - Ngorongoro Pastoral Council (Baraza la Wafugaji)