Naomba kujua je zile Tv zinazowashwa kila siku kwenye maduka ya Tv ukinunua utaiita mpya au used?

Naomba kujua je zile Tv zinazowashwa kila siku kwenye maduka ya Tv ukinunua utaiita mpya au used?

Used mpya.. 😀😀😀

Mimi huo upumbavu wao huwa naupingaga sana. ndio mana nikitaka kitu na tukisha afikiana bei nataka unitolee kitu nione kikikatwa seal na kutestiwa mbele yangu.
Wakisha itumia baada ya muda wanairudisha ndani ya boksi lake na kuifunga kama ilivyokuwa. Sio rahisi kwa mteja kung`amua kama ilikwisha wekwa kwenye Show! Hali kadhalika model husika inapokwisha na kubaki moja wanaipaki upya...
 
Wakisha itumia baada ya muda wanairudisha ndani ya boksi lake na kuifunga kama ilivyokuwa. Sio rahisi kwa mteja kung`amua kama ilikwisha wekwa kwenye Show!
Kwa sisi wapenda ligi tunazijua tu. kitu iliyotumika utaijua tu ikishafunguliwa.
 
Ila nichojifunza ni kuwa, Ukihitaji TV husika basi huenda kukuchukulia stoo, Ndivyo ilivyo kwa maduka ya hapa Kariakoo.

Mwl RCT, maduka makubwa ya Kariakoo utakuta Tv zaidi ya 10 zimewashwa kwa wakati mmoja, je unafikiri zote hizo hazitauzwa?
Wanachofanya ni baada ya muda wanazipaki kwenye maboksi yake na kuziweka stoo!
 
VITU VINGI VYA UMEME HUWA VINAFANYIWA MAJARIBIO YA KUVIWASHA ILI KUHAKIKISHA KAMA NI VIZIMA.
PIA KWENYE VIFAA KAMA TV VINAWASHWA VILE KUSUDI ILI UONE TOFAUTI YA UBORA WA RANGI NA MWONEKANO ILI IKURAHISISHIE KUCHAGUA AINA ULIYOIPENDA.
BINAFSI NAPENDA NINUNUE ILIYOWASHWA SABABU HATA HAO WAUZAJI WENYEWE WANAIAMINI NI ORIGINAL NDIO SABABU WAKATHUBUTU NA KUIAMINI KUIFANYIA MATANGAZO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kuna jamaa yangu Analinambia zile zinazowashwa muda mwingine ndio original then za stoo mi feki, so anachokifanya snachukua ile ya sample. Lakini wengine hawataki kutoa zile za sample

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlitakaje muuziwe TV zilizokuwa zipo tu kwenye mabox!
Mtavutiwaje Sasa
Gari yenyewe iliyopo showroom utaikuta iko tembea km 10
Sim yenyewe Ukienda nunua lazima aziwashe huko anaponunulia!

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia utaratbu huu,, mkishakubaliana bei,, mwambie akupe nyingine kutoka store ambayo haijafunguliwa,, sio kukuuzia hyo apo inayotumika kama demo

Wapendwa naomba kujua je zile Tv zinazowashwa kila siku kwenye maduka ya Tv (Demo), ukinunua utasema umenunua Tv mpya au iliyotumika (used)?
 
Nawashukuru kwa maoni na ushauri wenu, lakini nakiri baadhi huwashwa muda mrefu kiasi kuwa sawa na TV zilizotumika!!!
 
Mjadala Mrefu Naamini Ukweli Utajulikana
 
Wapendwa naomba kujua je zile Tv zinazowashwa kila siku kwenye maduka ya Tv (Demo), ukinunua utasema umenunua Tv mpya au iliyotumika (used)?
Zile ni sample, ukisema unataka hii wanaenda kukuletea kama hiyo kutoka store.
 
Hizo ni display ninavyojua kwa maduka ya nje huwa baada ya muda au model mpya zinapoingia huwa zinauzwa kwa pungufu kubwa na unaambiwa kabisa kuwa hii ilikuwa displayed kwa muda dukani na inauzwa kwa bei pungufu.

Sasa kama unataka bei poa hiyo ndio ya kuchukua
Kwa huko kariakoo kwa kweli sijui huwa wanauzaje hizo ingawa sisi kila kitu ni ujanja ujanja hata wapate faida kiasi gani bado watataka zaidi

Sent from my SM using Tapatalk
 
Back
Top Bottom