Ukiyasoma maneno haya na kuyatafakari utagundua walioyatoa na kuyaandika walikuwa na akili na waliona mbali. Lakini tunaweza tukawaendekeza wapumbavu wakatuletea kuchanganya dini na mamlaka ya nchi isiyo na dini. Tukiwakubalia ikatokea hivyo, tutavurugana sana na mwisho wa siku tutakuta hakuna mshindi. Watakaobahatika kuwa wamesalimika wakaishi watakaa watajadiliana wapi tumekosea na mwisho wa siku watarudi palepale kuwa mamlaka ya nchi yasichanganywe na ya dini, nchi yetu wananchi wake wana dini mbalimbali huo ndio ukweli, kamwe hautapingika, tupende tusipende utasimama kama si leo basi kesho.