pia inasemekana martin luther senior ktk kupitapita kwenye maktaba ya vitabu huko vatican ndipo alipokuta kitabu cheusi(biblia) kimening'inizwa kwenye minyororo, akajiuliza kwanini kitabu hicho cheusi kilizungushiwa minyororo, kumbuka wakati huo hakuruhusiwa mtu yeyote kusoma biblia isipokuwa tu papa na viongozi wa juu wa kanisa katoliki. Kwahyo Martin Luther akaifungua ile minyororo ili asome na kujua kitu gani kiliandikwa ndani, hapo ndipo aliposoma na kugundua kuwa kanisa lilikuwa likifanya mambo tofauti na biblia na ndiyo maana waliwatesa sana wakristo waliokuwa na msimamo mkali wa kufata kile kilichoandikwa kwenye biblia. Baada ya Martin luther kugundua ukweli huo akaamua kumpinga papa na kuanzisha dhehebu la lutheran(protestant).