Naomba kujua machache kuhusu biashara ya Chupa za Plastiki zilizotumika

Naomba kujua machache kuhusu biashara ya Chupa za Plastiki zilizotumika

Joined
Jan 22, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Wadau, ningependa kujua biashara ya kukusanya chupa za plastic zilizotumika kwa kuwa nimeona kuna fursa katika mkoa niliopo. Dar imekuwa dili sana naona watu wanabeba mizigo mikubwa ya machupa lakini huku nilipo chupa zinazagaa hakuna muokotaji.

Soko lake likoje? Wanunuzi wake ni akina nani? Wananunua kwa ujazo gani ni kwa kilo au na je kilo wananua shilingi ngapi?

Hapo kwenye bei ni muhimu ili hata ukiweka cost za usafirishaji zilete faida. Kama kuna mwenye ufahamu atujuze.
 
Yadaiwa pia kupunguza kwa kiasi kikubwa UHALIFU!

Angalizo - vijana tusidharau kazi, cha msingi ni mkono uende kinywani, kumbukeni kwamba tunakula ili tuishi!
 
"ANGALIZO" Lakini kazi hii siyo suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana.
 
Vijana wengi hao je wanaweza hata pita interview? Wakiwekwa wao na tuseme waKenya nani atachukuliwa?

Kuna mambo mengi lazima yapo, kama Lyimo unavyosema sio suluhisho ungesema Y as umeleta kama angalizo lako. Ila hauoni kuwa walioingia kwa hilo wamepunguza idadi ya wasio na ajira?
 
Last edited by a moderator:
yadaiwa pia kupunguza kwa kiasi kikubwa UHALIFU !

Nionacho mimi ni kundi kubwala vijana matejana walevi wa pombe ndiohuokota makopo, ni ajira ya kipuuzi kwani hulazimika hata kupekua uchafu ili kupata hizo chupa used, nishawahi kuwauliza kwa nn wengi wao wachafu na walevi wa unga na pombe, hujibu ni kupunguza aibu kwani kazi yakuzurula kutafuta chupa sio rahisi kwani zamani walikuwa wanaifanya machizi

Kwa mtazamo wangu ni hoja nyepesi kuon eti hii ni sehemu iliyoongeza ajia kwa vijana n liwe jambo la kujivunia, labda kama hukufikiri sawasawa au hujafanya hata kautafiti bali umelibeb tu.
 
Kukosa maarifa ni hasara sana. Kifupi ni kuwa mfumo uliopo ndo umewafanya vijana kujiingiza kwenye kazi kama hiyo. Tulipowanyang'anya nyumba wahindi ni kuwa tuliona mfumo wa kikoloni uliwafanya wao kunemeka kupitia jasho letu. Kwasasa serikali ya ccm imekosa vision kuwakwamua vijana, zaidi ya kuweka matabaka kwenye elimu, afya, usafiri n.k.

Angalia kwa umakini matokeo ya kidato cha nne mwaka huu je ni nani atakae okota makopo kama sio mtoto wa mkulima? Geodfrey Mgimwa ataokota kopo kweli wakati anjua kuwa atarithi ubunge wa baba yake?
 
Nionacho mimi ni kundi kubwala vijana matejana walevi wa pombe ndiohuokota makopo, ni ajira ya kipuuzi kwani hulazimika hata kupekua uchafu ili kupata hizo chupa used, nishawahi kuwauliza kwa nn wengi wao wachafu na walevi wa unga na pombe, hujibu ni kupunguza aibu kwani kazi yakuzurula kutafuta chupa sio rahisi kwani zamani walikuwa wanaifanya machizi
kwa mtazamo wangu ni hoja nyepesi kuon eti hii ni sehemu iliyoongeza ajia kwa vijana n liwe jambo la kujivunia, labda kama hukufikiri sawasawa au hujafanya hata kautafiti bali umelibeb tu

CHA KUSIKITISHA PAMOJA NA UKWELI KWAMBA NI MWEHU PEKEE ANAYEWEZA KUOKOTAOKOTA MACHUPA MAJALALANI , BADO tv 1 WAMEONA NI BIASHARA !
 
Kukosa maarifa ni hasara sana. Kifupi ni kuwa mfumo uliopo ndo umewafanya vijana kujiingiza kwenye kazi kama hiyo. Tulipowanyang'anya nyumba wahindi ni kuwa tuliona mfumo wa kikoloni uliwafanya wao kunemeka kupitia jasho letu. Kwasasa serikali ya ccm imekosa vision kuwakwamua vijana, zaidi ya kuweka matabaka kwenye elimu, afya, usafiri n.k. Angalia kwa umakini matokeo ya kidato cha nne mwaka huu je ni nani atakae okota makopo kama sio mtoto wa mkulima? Geodfrey Mgimwa ataokota kopo kweli wakati anjua kuwa atarithi ubunge wa baba yake?

Kwi! Kwi! Kwi! Mkuu hujang'ata maneno , asante sana .
 
"ANGALIZO" Lakini kazi hii siyo suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana.

MKUU kiukweli HAKUNA YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU ANAYEWEZA KUOKOTA CHUPA BARABARANI , WENGI NI WEHU TU !
 
Jamani wanaojua watwambie, japo mi nina ushaidi, kuna jamaa mmoja alikuja Dar, akiwa amelenga kufanya biashara hii, ameanza mdogo mdogo tu, mtaji ulipokuwa akaanza na biashara ya chuma chakavu. Kwasasa jamaa kaajiri watu kutokana na biashara hii, yuko vizuri kimaisha, ana nyumba tatu mbili anapangisha, duka la jumla na pikipiki. Mambo yanamnyookea.

Lkn anasema hiyo biashara hatoiacha kamwe hadi pale god atakapomchukua, kwa hiyo ukiwa na nia na kujituma katika jambo lolote halali hakika utafanikiwa.
 
acheni stori za vijiweni, hiyo biashara ni kichaa vibaya mno....huko viwandani kwenyewe wananunua kilo moja kwa TZS 400-500...sasa shughuli yake mpaka chupa tupu zifike kilo kazi ipo...labda uzijaze maji ndo uzito kidogo uongezeke
 
Mkuu unaweza kuajiri vijana watatu tu, unawawekea malengo kwa siku wazungu ke sehemu mbalimbali jijini dar labda gunia mbilimbili kwa siku piga hesabu kwa mwezi ni chupa ngapi, wawe wana mwaga kwako, uone kama hujanufaika.
 
acheni stori za vijiweni, hiyo biashara ni kichaa vibaya mno....huko viwandani kwenyewe wananunua kilo moja kwa TZS 400-500...sasa shughuli yake mpaka chupa tupu zifike kilo kazi ipo...labda uzijaze maji ndo uzito kidogo uongezeke

Unapenda kazi laini. Kubofya computer hela zije, hizo chupa zinakusanywa mpaka inafika tani, watu wanakusanya tani 20 per day unafanya mchezo.
 
Jamani sasa utafanye biashara ya ku recycle plastic ambazo zinazagaa mtaani kama huna waokota makopo,tuheshimu kazi za watu tafadhari tunawahitaji sana ili wapunguze uchafu mitaani na pia ni surce ya ajili ,assume umepata tenda na bakresa ya kuwauzia chupa za plastic kilo tsh 10,000/= utafanyaje.
 
Jamani sasa utafanye biashara ya ku recycle plastic ambazo zinazagaa mtaani kama huna waokota makopo,tuheshimu kazi za watu tafadhari tunawahitaji sana ili wapunguze uchafu mitaani na pia ni source ya ajira ,assume umepata tenda na bakresa ya kuwauzia chupa za plastic utafanyaje.
 
Mambo VP wakuu.. Nilikuwa naomba idea kwa mwenye uwelewa juu ya hii biashara ya kuuza plastics zilizosagwa.

1. Bei ya mashine ya kusaga Chupa za plastics, na installation yake kama umeme wa 3phase au single

2. Upatikanaji wa chupa za plastics na bei zake

3. Masoko yake na bei zake kwa kg1

4. Na changamoto zake...
 
Back
Top Bottom