Naomba kujua machache kuhusu biashara ya Chupa za Plastiki zilizotumika

Naomba kujua machache kuhusu biashara ya Chupa za Plastiki zilizotumika

Habari wakuu .nahitaji kukusanya plastics zilizotumika km vile chupa za plastics ndoo zilizochakaa au kupasuka na kuziuza baadae kwa mwenye uzoefu na hii biashara ningependa anisaidie inavyofanyika biashara na changamoto zake .naomba kuwasilisha
 
Ndugu zangu mtafutaji hachoki. Naomba msaada wenu kwa yeyote aliyewahi kufanya biashara ya kuuza chupa tupu za plastiki zilizotumika.

Bei ya wanunuzi viwandani, majina ya viwanda na eneo wanakopatikana.
Najua soko kubwa lipo DSM.

Natanguliza shukrani kwa atakaetoa ushauri wake. Asanteni
 
survivor03, Kuna mashine ya mil 5, mil 6, mil 7 mpk 10 n.k

Unaweza nunua za tz ama uka agiza toka china.

Umeme unaweza weka wa 2000 ukasaga chupa kuanzia kg 100-120kg/1hr, inategemea na mashine yenyewe.

Masoko yapo yan ukishachakata masoko yapo ya kutosha.. bei ya kuuza inatofautiana chupa nyeupe ina bei zake, vizibo pia ina bei yake n.k

Ili uone faida yake vzur nilishauriwa nikusanye sio chini ya tan moja za chupa.

Bei ya kununua chupa ni around 250tsh na chupa za energy drnk inakuwa chini kidogo, hii bei inaweza kuwa tofaut sehem moja mpk nyingne.

#niko busy kidogo so chukua hata haya machache
 
Pia, usianze biashara hii kama hauna uhakika wa kupata chupa kwa wingi,

pia chupa zilizopo mtaani kwako zisikudanganye zitatosha hapana,

Kwahyo chakufanya hakikisha una tafuta eneo kwanza weka uzio then kusanya chupa kwanza then uone rate yake, ukiona rate ni kubwa na umekusanya mzgo wa kutosha ndio uende kwenye step ya kununua mashine,

Ukitenga eneo then ukakusanya chupa ukaona rate itakuwa ndogo unaweza ziuza kwa wengine so utaepuka hasara kiasi flan
 
Huku kwetu watoto wanapasua hizo chupa kutoa ile mikanda ya kushikia vizibo
 
Habari wakuu .nahitaji kukusanya plastics zilizotumika km vile chupa za plastics ndoo zilizochakaa au kupasuka na kuziuza baadae kwa mwenye uzoefu na hii biashara ningependa anisaidie inavyofanyika biashara na changamoto zake .naomba kuwasilisha
inafuatana unataka kufanyia wap, mm nmeshaanza kuifanya iko vizuri sana
 
survivor03, Kuna mashine ya mil 5, mil 6, mil 7 mpk 10 n.k

Unaweza nunua za tz ama uka agiza toka china.

Umeme unaweza weka wa 2000 ukasaga chupa kuanzia kg 100-120kg/1hr, inategemea na mashine yenyewe.

Masoko yapo yan ukishachakata masoko yapo ya kutosha.. bei ya kuuza inatofautiana chupa nyeupe ina bei zake, vizibo pia ina bei yake n.k

Ili uone faida yake vzur nilishauriwa nikusanye sio chini ya tan moja za chupa.

Bei ya kununua chupa ni around 250tsh na chupa za energy drnk inakuwa chini kidogo, hii bei inaweza kuwa tofaut sehem moja mpk nyingne.

#niko busy kidogo so chukua hata haya machache
Mkuu nimekuelewa sana idea yako.
Naomba kujua mahitaji yote na jumla ya mtaji ambao mtu anatakiwa kuanza nayo ili kufanikisha hiyo biashara ya kusaga chupa ili mtu asije kukwama na kuishia njiani?
Na je ni nani anayenunua hizo chupa zilizosagwa?
 
Huku kwetu watoto wanapasua hizo chupa kutoa ile mikanda ya kushikia vizibo
Nazani hii kitu wanafunsishwa kwn somo la stad zakazi mashuleni japo sina uhakika,hiyo mikanda yavizobo wanatengezea kamba flani ivi kwa kuunganisha unganisha kwa ustad kdg wakumix rangi mbali mbali,kuna mmoja nilimuuliza izo kamba mnafanyia nini akasema unaweza ata kuachikia pazia
 
Mkuu nimekuelewa sana idea yako.
Naomba kujua mahitaji yote na jumla ya mtaji ambao mtu anatakiwa kuanza nayo ili kufanikisha hiyo biashara ya kusaga chupa ili mtu asije kukwama na kuishia njiani?
Na je ni nani anayenunua hizo chupa zilizosagwa?
Kama hautojal utanichek pm nikupe maelezo.. huku nasahau kutembelea ndio maana leo ndio nmeona reply yako. Usiogope kuniulza PM nitakupa maelezo bure kabsa.
Nmefanya hvyo ili nikumbuke
 
Mambo VP wakuu.. Nilikuwa naomba idea kwa mwenye uwelewa juu ya hii biashara ya kuuza plastics zilizosagwa.

1. Bei ya mashine ya kusaga Chupa za plastics, na installation yake kama umeme wa 3phase au single

2. Upatikanaji wa chupa za plastics na bei zake

3. Masoko yake na bei zake kwa kg1

4. Na changamoto zake...
1. Bei ya machine inacheza kwenye milion 8-milion 16 zinapatkina kwa wachina wenyewe au unaweza kuagiza nje, SIDO wanauza lakn Visu vyake sio imara zinawah kuharibika, umeme ata single
2. upatikanaji wa chupa wanaokuletea ni vijana sana sana ni mateja, unafungua kijiwe wenyewe wanakuwa wanaleta kijiwen kwako unawalipa
3. Masoko yako mengi sana sana wanunuaji ni wachina na wapo sehem tofauti kwa dar kuna kiwanda kipo Mbezi Makonde, kingne kipo Gereji kama unaenda tabata, vingine vipo kurasini. kiwandan kwa kilo ambayo aijasagwa inacheza kwenye 400 -500 kwa iliyosagwa inacheza kwenye 1,000 per kg
4. Changamoto zake upatikanaji wa chupa kwa dar ni mgumu make wanunuaji ni wengi alaf pia wanaokuuzia chupa hawatabirki wanaweza kuja kwako wakaleta mzigo wakajaza ata maji kwa chupa ili mzigo uwe na kilo nying ukijifanya kuwazingua wanakuama, so unakua unahangaika na kupatikana kwa mzigo,
hayo ndo machache ninayoyajua
 
Wadau, ningependa kujua biashara ya kukusanya chupa za plastic zilizotumika kwa kuwa nimeona kuna fursa katika mkoa niliopo. Dar imekuwa dili sana naona watu wanabeba mizigo mikubwa ya machupa lakini huku nilipo chupa zinazagaa hakuna muokotaji. Soko lake likoje? Wanunuzi wake ni akina nani? Wananunua kwa ujazo gani ni kwa kilo au na je kilo wananua shilingi ngapi? Hapo kwenye bei ni muhimu ili hata ukiweka cost za usafirishaji zilete faida. Kama kuna mwenye ufahamu atujuze.
Ulishapata ufumbuzi mkoa uliopo wa hayo machupa
 
Viwanda vipi ununua chupa
acheni stori za vijiweni, hiyo biashara ni kichaa vibaya mno....huko viwandani kwenyewe wananunua kilo moja kwa TZS 400-500...sasa shughuli yake mpaka chupa tupu zifike kilo kazi ipo...labda uzijaze maji ndo uzito kidogo uongezeke
 
Mkuu unaweza kuajiri vijana watatu tu, unawawekea malengo kwa siku wazungu ke sehemu mbalimbali jijini dar labda gunia mbilimbili kwa siku piga hesabu kwa mwezi ni chupa ngapi, wawe wana mwaga kwako, uone kama hujanufaika.

Sababu ya Corona bei imeshuka waokotaji uuza kilo sh 50 Hadi 100 wasagaji wanunua kwa 150 Hadi 200 kwa kg wakishasaga uuza kiwandani kwa 350 Hadi 450.
 
Ndugu zangu mtafutaji hachoki. Naomba msaada wenu kwa yeyote aliyewahi kufanya biashara ya kuuza chupa tupu za plastiki zilizotumika.

Bei ya wanunuzi viwandani, majina ya viwanda na eneo wanakopatikana.
Najua soko kubwa lipo DSM.

Natanguliza shukrani kwa atakaetoa ushauri wake. Asanteni
Vipi ulishapata majibu
 
Sababu ya Corona bei imeshuka waokotaji uuza kilo sh 50 Hadi 100 wasagaji wanunua kwa 150 Hadi 200 kwa kg wakishasaga uuza kiwandani kwa 350 Hadi 450.
Kwaiyo tani mmoja kiwandani ni 450k.
( apo bado usafiri na wapikiaji)

Hii tani mmoja ukusanyaji wake si sio mchezo sasa. Waweza chukua siku ngapi.

Kwaiyo mtaji wake kwa hesabu zako ni laki 100k_200k. Si ndivyo mkuu.
 
Back
Top Bottom