1. Well, kwa kiasi kikubwa mishahara ya Serikalini inatofautiana sana. Kuna watu wanafanya kazi Serikalini lakini mishahara yao, posho na mazingira yao ya kazi ukiwalinganisha na watumishi wengine unaweza kudhani hii si nchi moja.
2. Kwa ujumla, watumishi wa umma wanaofanya kazi kwenye Halmashauri za Wilaya, Manispaa, Majiji na Wizarani wanatumia scale za mishahara kwa mfumo wa TGS, ambao naweza kusema wanalipwa mishahara midogo kulinganisha na wengine nitakaowaelezea katika point namba 4 hapa chini. Hawa mara nyingi mtu wa degree anaweza kuanza na basic ya 710,000/= au 715,000/= hivi. Hata hivyo, mishahara yao hupanda kila baada ya miaka kadhaa (mara nyingi kila baada ya miaka 3). Huku ndio kunaitwa kupanda madaraja ambako awamu iliyopita iliwanyima hiyo haki yao ya kupanda hayo madaraja kama utakavyokuwa unasikia kelele nyingi huku mitandaoni wanavyosema.
3. Kwa mantiki hiyo, mtumishi anayeanza kazi leo katika level ya degree si sawa na yule mwenye miaka 6 au 9 au 12 kazini. Unaweza kukuta mtu baada ya miaka kadhaa kapandishwa madaraja na analipwa mshahara kufikia hata 1.5M au hata 2M.
4. Kama nilivyosema hapo juu kwenye point namba 2, huko serikalini, watumishi wa umma wanaitumikia Serikali moja ila kupitia njia (Waajiri) au channel tofauti tofauti ambazo zinatofautiana kwa kiasi kikubwa sana. Mshahara na posho za Mtumishi wa Local governament (maarufu kama Halmashauri) si sawa kabisa na Mtumishi wa Mashirika au Taasisi nyingine za Serikali kama vile TANESCO, EWURA, TPDC, HESLB, BOT, TRA, TANAPA, TCRA, VYUO VIKUU, OFISI YA CAG, BRELA, NIMRI, n.k. Watumishi wa hizi Taasisi kwa mazingira ya kazi zao, mishahara yao na posho za hapa na pale, kiufupi unaweza sema wanafanya kazi kwenye private sectors tena zinazosimamiwa na viongozi kutoka nchi za nje. Ila ndio hivyo wote tupo nchi moja. Ukifuatilia kwa undani utajua pia ni kwa nini kuna huo utofauti. Kama unabisha wewe nenda ofisi za NIMRI pale POSTA- DAR, au nenda Ofisi za HESLB- Mwenge, au TCRA - Ubungo Mawasiliano halafu uende na Ofisi ya Manispaa ya Temeke au Ilala uone kama hata tu mazingira ya Ofisi zao kama yapo sawa kisha ulete hapa mrejesho.
4. Jambo lingine linalowapeleka watu Serikalini ni ukweli kuwa huko kuna security kubwa ya kazi ukilinganisha na private sector. Maana yake ni kuwa, ukiwa mtumishi wa umma, hata ukifanya makosa, kuja ukaachishwa kazi process zake ni nyingi kidogo na si rahisi kama ilivyo kwenye private sector ambako unaweza kuwa na kazi leo na wiki ijayo ukawa jobless.
5. Ukweli mwingine ni kuwa, mbali na mishahara, watumishi wengi wa Serikalini wanapata posho za hapa na pale kutokana na extra duties, perdiems za safari kikazi, trainings n.k zinazowaweka mjini. Ndio umesikia pia juzi kuwa zimepandishwa. Kabla ya kupandishwa juzi, mtu wa degree alikuwa anapata posho ya kujikimu laki moja kwa siku akienda safarini kikazi katika sehemu za mikoani au majiji. Sasa unaweza kuta mtumishi ana visafari vya hapa pale kwa mwezi angalau hata mara moja, au akikosa sana ndani ya miezi mitatu hakosi kasafari. Sasa akipata 100K kwa siku mara siku 7 tu tayari ana 700K. Unaona sasa Mkuu?
6. Mtumishi wa Serikalini ana fursa ya kujiendeleza kielimu na akiwa masomoni, ataendelea kupokea mshahara wake na kazi yake akirudi ataikuta. Kitu ambacho ni kigumu sana kwenye Private sectors.
7. Mtumishi wa Umma mbali na fursa ya matibabu kwa BIMA yeye na familia yake ikiwamo wazazi wake, ana fursa ya kuweza kukopa mkopo kwa njia rahisi ukilinganisha na yule wa Private sector.
Kimsingi hizo ni baadhi ya sababu zinazowafanya watu kukimbilia huko Serikalini licha ya mishahara ya kuanzia kuwa midogo ukilinganisha na private sectors.