Naomba kujua namna Islamic Banking inavyopata faida

Unafanywaje?
 
Ni jinsi gani benki za kiislamu zinatengeneza mzigo.

Iko hivi benki zinatoa mikopo bila riba, ila itatakiwa mchukuwa mkopo afanye makubaliano na benki husika ya kugawana faida
 
Mambo muhimu hasa kuhusu Islamic banking ni;
1. Uislam hauruhusu mkopo wa bidhaa fulani kwa marejesho ya mara dufu ya bidhaa hiyo hiyo.
Mifano: mkopo wa fedha sh. 100 ili kurejesha sh. 150, au mkopo wa karanga ndoo 2 ili kurejesha karanga ndoo 3 hii ni haram ktk Islam.
Ila kukopa printer ya sh. 100 ili urejeshe sh. 2,000 na mikopo mingine yenye mpishano wa aina za bidhaa halali ndio uislam.

2. Uislam ni kuamin kuwa wajibu wetu ni kazi na swala/dua ila riziqi (kupata/kukosa) inatoka kwa Allah (uncertainty inazingatiwa na wote, bank na mteja) hivyo, mgawo wa faida kati ya Islamic bank na mteja unazingatia asilimia/percent na si kuweka kiwango maalum. Yaani, Islam inataka bank na mteja washirikane kwenye faida na hasara, tofauti na bank zisizo za kiislam ambazo mteja unahakikishiwa leo kwamba mwakani December utavuna million 5 bila kujali bank inapitia vipindi vya faida na hasara hapa kati.

3. Islamic banking haziwekezi kwenye biashara haram kama pombe/vilevi, kamali, burudan za utupu, kilimo haram na ya kama hayo.


البقرة (275) Al-Baqara

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

~Naomba wajuzi zaidi yangu wanikosoe na/au kuongeza~
 
Kiongozi biashara unajua japo kidogo? Je faida na riba ni sawa?
 
Kumbe ndio wajanja hivi hahahaaaaa
 
Unafanywaje?
Labda nimjibie Katika uislam kama ukishindwa kulipa deni inaangaliwa ni kwanini hujalipa lile deni ilionekana kuwa huna uwezo nalo uislamu unamafungu manane ya wanaotakiwa kupewa zaka miongoni mwao ni wenye madeni sugu walioshindwa kulipa hivyo utalipiwa deni lako kutoka kwenye fungu hilo ila ikionekana unafanya makusudi sheria itafuata mkondo wake
 
Hivi Islamic banks hawachukui dhamana wakikopesha?
 


Kama wanafanya hivyo hiyo ni riba.
 
Hivi Islamic banks hawachukui dhamana wakikopesha?
Dhamana yao ni hivyo walivyokupa ufanyie biashara/ujijenge. Uki default njiani, na wao ni hasara kwao. Ndio maana Islamic bank hawakupi pesa bali wanakufanyia icho unachotaka. Wao mara zote wanataka ufanikiwe ili wajilipe chao, maana wanajua ukipata hasara, na wao kwao ni hasara, hawaji kukuchukulia nyumba yako.

Pia unapoona kuwa huwezi kulipa kwa kile kipindi ambacho mmekubaliana na unahitaji mda, wakijiridhisha hasa kuwa ni kweli mambo magumu, basi wanatakiwa wakuongezee mda tena bila ya penalty. Ila ukiwa hujalipa kwa awamu mlizokubaliana na ukakosa sababu ya msingi wana haki ya kukutoza adhabu.

Sasa kwenye bank zetu za kawaida ni vice versa ya hio model. Kwanza kiukweli, mabenk wanataka watu waendelee kuwa kwenye madeni tu, ili wawatoze izo RIBA. Wewe ukifanikiwa usifanikiwe wao wanakuja kuchukua dhamana ulizoweka.
 
Hiii imekaa vzr, je masharti ni lzm uwe muislam? au vigezo vyao vikoje
 
Hiyo ni riba wanakwepa neno riba ila wana riba kubwa sana
 
Kiufupi wanatoza riba (tena kubwa tu) ila kwa mtindo tofauti ikiwemo kuweka kona kona, ujanja ujanja wa maneno na kujitahidi kuipa jina tofauti hiyo riba.

Kama hujaelewa, embu jaribu kutafakari tofauti ya Nguruwe, Kitimoto, Mdudu na Mbuzi katoliki.
Ulishawahi kupata mkopo wa aina inayozungumziwa?
Wanachofanya wanaingia ubia na mkopaji alafu wao wanakua kama financial management na wewe unasimamia kazi zingine. Na faida au hasara mnagawana kwa mahesabu yaliopigwa.
 
Naona upenyo wa kuitapeli benki kwa hiyo njia yao ya wewe kuwaelekeza muuzaji kisha wao waende kununua halafu wakukabidhi wewe.
 
Naomba kujua mfumo wa Islamic Banking unapataje faida kama wao hawatozi riba? Kama hawana riba wanalipaje wafanyakazi na kukodi majengo? Nakopa million 100 narudisha milioni 100 hapa mtaji unakua vipi?
majini mengi yanaleta pesa
 
Hiii imekaa vzr, je masharti ni lzm uwe muislam? au vigezo vyao vikoje
Sio lazima uwe muislam. Kuna bank ambazo sio za kiislam lakini zina account yenye kufuata izo taratibu, ndio uombe ufunguliwe hio. Haijaalishi upo dini, mfumo upo kwa kila mmoja.
 
Sio lazima uwe muislam. Kuna bank ambazo sio za kiislam lakini zina account yenye kufuata izo taratibu, ndio uombe ufunguliwe hio. Haijaalishi upo dini, mfumo upo kwa kila mmoja.
Ahsante kwa kunielewesha Mkuu
 
Hakuna mkopo usiyokuwa na riba

Ova
 
Kwa kifupi inabidi umkabidhi mtu sehemu ya akili yako akusaidie kufikiri ndiyo uamini kuwa hawana riba. Mtu unahitaji gari la tsh 10m badala wakupe 10m ukanunue gari ili uwarudishie 10m baada ya muda(hii ndiyo maana halisi ya interest free), wao wanakupiga sound na blaah blaah nyiingi alafu wanakununulia hilo gari wanakukopesha kwa 12m alafu unakuta mtu anashangilia kuwa hajalipa riba.
 
Kwa kifupi inabidi umkabidhi mtu sehemu ya akili yako akusaidie kufikiri ndiyo uamini kuwa hawana riba. Mtu unahitaji gari la tsh 10m badala wakupe 10m ukanunue gari ili uwarudishie 10m baada ya muda(hii ndiyo maana halisi ya interest free), wao wanakupiga sound na blaah blaah nyiingi alafu wanakununulia hilo gari wanakukopesha kwa 12m alafu unakuta mtu anashangilia kuwa hajalipa riba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…