Naomba kujua namna Islamic Banking inavyopata faida

Naomba kujua namna Islamic Banking inavyopata faida

Ukitaka tende za madina ilhali wewe unazo za maka basi uza zako za madina ili ununue za maka uki exchange tende kwa tende basi hiyo ni riba.
 
Nipo Mwanza kabla ya kurudi Tarime,kesho naenda kuwaona nipate uhalisia.Nitaleta mrejesho hapa jamvini.
 
Huo Ndo ukweli.Inajulikana there is quite difference btn Profit and Interest lakini wao wanatumia interest kwa jina la Profit.Mfano kwa interest (riba)Nikimkopesha MTU sh.100 kila mweI unaozidi nikimwambia atalipa 50 akaja lipa baada ya miezi 5 itaongezea kwa 50.But profit wherever itaremain tuliyokubaliana.Hata ipite miezi 5 nitalipa iyo 150,50 kama faida haiongezeki.Sasa wao wanatumia njia za interest (Riba)kwa mgongo wa Profit(faida)Na hawakopeshi pesa wao Ni materials kama mdau mmoja alivyofafanua .Huyo aliyesema Milioni 100 atalipa 100 .Nothing like that .
Watakwambia mambo haya:

Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.

Kwa mfano:

Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.

Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonesha (kukuzuga) kuwa riba na faida ni kitu tofauti kwa kuwa Uislamu hauruhusu riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'Kswahili kiswahili'.
 
Kwanza hizo pesa utazipata wapi?ukitaka million 100 wataenda kukufanyia kitu cha million 100.pesa mwiko
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?

Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?
 
Back
Top Bottom