Hazchem plate
JF-Expert Member
- Feb 25, 2011
- 11,048
- 15,465
Unapigiwa dua ya mauti
Ukiacha kulipa deni unafanywaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiacha kulipa deni unafanywaje?
Au unasomewa albadiri unavuta fasterUnapigiwa dua ya mauti
Watakwambia mambo haya:
Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.
Kwa mfano:
Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.
Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonesha (kukuzuga) kuwa riba na faida ni kitu tofauti kwa kuwa Uislamu hauruhusu riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'Kswahili kiswahili'.
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?
Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?