Watakwambia mambo haya.
Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.
Kwa mfano.
Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.
Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonyesha(kukuzuga!) kuwa Riba na Faida ni kitu tofauti kwa kuwa uislamu hauruhusu Riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'kiswahili kiswahili'.