- Tambua chuo na program zinazotolewa kama zinaendana na masomo uliyosomea.
- Angalia unaomba kama nani?! Tutorial Assistant (ukiwa na Bachelor degree) au Assistant Lecturer (Masters degree) na kadhalika, bila kusahau vigezo vyake.
- Andika barua rasmi ya kiofisi kuulizia kama kuna nafasi ya kuhamia kwa cheo na eneo la utaalamu kwenye hicho chuo.
Kama mabosi wako sio wanoko, unaweza kuipitishia kwao kuongeza mkazo zaidi. Hili huwa ni lazima, japo unaweza kufanya kimya kimya.
Mara nyingi vyuo hutangaza nafasi za kuhamia pia. Hii ni nafasi nzuri zaidi, maana huelekeza hadi namna ya kuomba kuhamia, japo process sio ngumu.
- Baada ya kuandika barua ya kuulizia nafasi ya kuhamia, kaa utulie usubiri majibu. Utajibiwa kwa maandishi na utaratibu wote utapewa, lakini mara nyingi utaelekezwa kuandika barua rasmi ya kuomba kuhamia hiyo taasisi. Utaiaddress hii barua kwenda utumishi, ukiambatanisha barua uliyojibiwa na taasisi kua kuna nafasi ya kuhamia.
Barua hii lazima ipitie kwa mwajiri wako wa sasa, akipitisha kwa kukubali ombi lako, imeisha hiyo mzee.
- Hadi hapo, utasubiri tu barua ya uhamisho toka utumishi, halafu unaenda kureport kituo kipya cha kazi.
Kama kuna upungufu wowote katika maelezo yangu, wadau wataongezea kukupa mwongozo zaidi.