Mimi kwangu huwa natumia air fresheners za kuchomeka kwenye soketi za umeme na ambazo ninaweza kudhibiti kiasi cha marashi yatokayo.
Baadaye nitaweka picha hapa muone nachozungumzia.
Jingine ni kutumia scented candles. Napendelea zaidi brand ya Yankee Candle.
Na huwa sipendi kupika vyakula vyenye shombo kali kama vile kukaanga samaki na kadhalika.
Nikikaanga samaki huwa nakaangia nje kwenye deck.
Halafu huwa napendelea zaidi marashi ya fresh na citrus.
Usafi wa nyumba nao husaidia pia. Hakikisha nyumba yako ni safi na yenye kuingiza na kutoa hewa vizuri.